Wednesday, 26 March 2025

TANGAZO LA KUHUSU TUZO ZA BURUDANI MBEYA

Tunapenda kuwajulisha wadau wote wa burudani kwamba upigaji kura kwa ajili ya Tuzo za Burudani Mbeya umekamilika rasmi! Tunashukuru kwa michango yenu na ushiriki wenu kwa kuunga mkono vipaji vya wasanii, wachekeshaji, wachezaji, waandishi wa habari, na wanamuziki.

Utaratibu wa ukabidhishaji wa tuzo hizi utaanza

kutangazwa rasmi katika wiki ya kwanza ya mwezi wa nne. Washindi na washiriki wote watapata fursa ya kutambulika na kuthaminiwa kwa michango yao katika sekta ya burudani.

BURUDANI MBEYA inajivunia kuwa jukwaa muhimu linalounganisha wasanii na mashabiki wao kupitia blog, YouTube channel, na Instagram page.

Shukrani kwa wote walioshiriki katika kura na kuonyesha mapenzi yao kwa wasanii wetu. Tunaamini tuzo hizi zitaongeza kasi ya ukuaji wa burudani na kutoa nafasi kwa vipaji vipya kuonekana.

Tuzo za Burudani Mbeya – Kuanza kwa mafanikio makubwa kwa wasanii wa Nyanda za juu kusini na Tanzania kwa ujumla!

Kwa maelezo zaidi:-

Email: burudanimbeya@gmail.com

Au tembelea:-

Web:www.burudanimbeya.blogspot.com

YouTube: Burudani Mbeya

0 comments:

Post a Comment