Kadri siku zinavyosogea kuelekea EASTER COMEDY SHOW tarehe 20 Aprili 2025 katika Tughimbe Hall, Mbeya, mashabiki wa vichekesho wanapaswa kujiandaa vilivyo ili kufurahia tamasha hili kikamilifu. Hapa kuna vidokezo muhimu kwa mashabiki wanaotegemea kuhudhuria:
1. KATA TIKETI YAKO MAPEMA
Epuka usumbufu wa dakika za mwisho kwa kununua tiketi yako mapema. Kumbuka bei za tiketi ni:
Regular – TSH 10,000
VIP – TSH 20,000
Special Seat – TSH 50,000
Meza ya watu 5 – TSH 250,000
Piga simu au WhatsApp 📞 0762446265 ili kupata tiketi yako sasa!
2. VA NGUO NZURI NA NZURI ZA KUSTAREHE
Utakaa kwa muda mrefu ukifurahia show, hivyo hakikisha unavaa mavazi mazuri na ya kustarehe. Ukiwa na Special Seat au VIP, unaweza kwenda na mavazi rasmi kidogo kwa ajili ya muonekano wa kifahari! (Hata regular pia)
3. NENDA MAPEMA ILI UPATE NAFASI BORA
Mlango utafunguliwa saa 12:30 jioni, hivyo fika mapema ili usipate usumbufu wa kusubiri foleni au kupoteza nafasi nzuri ya kukaa karibu na wasanii.
4. ENDA NA MARAFIKI AU FAMILIA KWA BURUDANI ZAIDI
Vichekesho ni vizuri zaidi ukivifurahia na watu wako wa karibu! Panga kwenda na washikaji au familia yako ili kufurahia pamoja na kusherehekea Pasaka kwa mtindo wa kipekee.
5. FOLLOW INSTAGRAM KWA UPDATES ZAIDI
Usipitwe na matangazo na mambo mapya kuhusu tamasha hili. Fuata ukurasa rasmi wa tamasha hapa 👉 @standupComedy_mbeya kwa taarifa za papo hapo.
6. KUWA TAYARI KUCHEKA HADI MBAVU ZIUME!
Weka mood yako tayari kwa kicheko cha kufa mtu! Wasanii waliopo ni wakali wa vichekesho, na watakupa burudani ya kiwango cha juu. Hakikisha unakuwa tayari kwa show ya mwaka!
Siku inakaribia – Jiandae kufurahia!
0 comments:
Post a Comment