Saturday, 29 March 2025

BURUDANI MBEYA AWARDS 2025: MFUMO WA KUMPATA MSHINDI

Mchakato wa kumpata mshindi katika Burudani Mbeya Awards umefuata hatua hizi:

1. Kukusanya Kura

- Mashabiki walipiga kura kwa njia ya mtandaoni (Google form).

- Kamati ya wataalamu (academy) nayo imetoa kura zake kwa kutumia vigezo na taratibu.

2. Kuhesabu Asilimia

Kwa kila mgombea, hesabu zinafanyika kwa kutumia fomula hii:

-          Alama za Mashabiki = (Kura za mgombea ÷ Jumla ya kura za mashabiki) × 85

-          Alama za Academy = (Kura za mgombea ÷ Jumla ya kura za academy) × 15

-          Jumla ya Alama = Alama za Mashabiki + Alama za Academy

3. Kupata Mshindi

Mgombea mwenye jumla ya alama nyingi zaidi ndiye anayeshinda tuzo husika.

Mfano wa Hesabu kwa Washindi wa Burudani Mbeya Awards

Ili kuelewa vizuri jinsi washindi wa Burudani Mbeya Awards wanavyopatikana, tuangalie mfano wa mgawanyo wa kura kwa wagombea watatu kwenye kategori ya Msanii Bora wa Mwaka:

Mgombea

Kura za Mashabiki

Kura za Academy

A

10,000

30

B

7,000

50

C

5,000

20

 

Hesabu kwa Mgombea A:

-          Alama za Mashabiki = (10,000 ÷ 22,000) × 85 = 38.64

-          Alama za Academy = (30 ÷ 100) × 15 = 4.5

-          Jumla ya Alama = 43.14

Hesabu kwa Mgombea B:

-          Alama za Mashabiki = (7,000 ÷ 22,000) × 85 = 27.05

-          Alama za Academy = (50 ÷ 100) × 15 = 7.5

-          Jumla ya Alama = 34.55

Hesabu kwa Mgombea C:

-          Alama za Mashabiki = (5,000 ÷ 22,000) × 85 = 19.32

-          Alama za Academy = (20 ÷ 100) × 15 = 3

-          Jumla ya Alama = 22.32

Katika mfano huu, Mgombea A ndiye mshindi kwa kuwa ana 43.14 alama, akifuatiwa na B (34.55) na C (22.32).

UMUHIMU WA MFUMO HUU KATIKA BURUDANI MBEYA AWARDS

Mfumo huu umehakikisha kwamba:
mashabiki wanakuwa na nguvu kubwa ya kuamua mshindi, kwa kuwa kura zao zinachangia 85% ya alama.
Ubora wa kazi unazingatiwa, kwani wataalamu wa burudani wanatoa maoni yao kwa kutumia vigezo vya kitaaluma.
Matokeo yanakuwa ya haki na yenye uwazi, kwa sababu kila mgombea anapata nafasi sawa ya kushindania tuzo.

Tukutane April 2025 kwa utaratibu zaidi wa utangazaji wa washindi kwenye kila Category.

@BURUDANI MBEYA


0 comments:

Post a Comment