Wounded
Healers Organization inakukaribisha katika mfululizo wa vikao maalumu vya
elimu, mjadala na ushauri wa kitaalamu juu ya afya ya akili na changamoto za
kisaikolojia zinazowakumba wasanii na wanamichezo.
Huu ni mwaliko wa pekee kwa wote wanaotaka kujifunza, kushirikiana na kupata
msaada wa kisaikolojia ili kuimarisha ustawi wa kiakili na ubunifu wao.
¾ Siku: Kila Jumapili kuanzia 24 Agosti 2025
¾ Muda: Saa 9 Alasiri – Saa 11 Jioni
¾ Mahali: Wounded Healers Organization HQ, Forest Mpya – My Choice Street
¾ Ada: BURE (Hakuna gharama ya ushiriki)
MALENGO
- Kuelimisha kuhusu aina na dalili za matatizo ya akili yanayoweza kuathiri wasanii na wanamichezo.
- Kujadili mbinu za kudhibiti matatizo ya akili, presha ya kazi na changamoto za kijamii.
- Kujenga mtandao wa msaada kati ya wasanii, wanamichezo na wataalamu wa afya ya akili.
- Kutoa nafasi ya faragha na ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu wa saikolojia.
JINSI YA KUSHIRIKI
Tuma ujumbe wenye neno "NITASHIRIKI"
kwa namba 0764 901 969 / 0757 741 013
Au tuma barua pepe kupitia: woundedhealersorg@gmail.com
Instagram: @wounded_healers_organization
KAULI
"Afya ya akili ni msingi wa ubunifu na ushindi. Karibu tuelimishane, tuzungumze, na tujenge afya bora ya akili kwa wasanii na wanamichezo."
WOUNDED HEALERS ORGANIZATION - COUNSELING HOME
0 comments:
Post a Comment