Monday, 5 May 2025

FUN RUN – RIFT VALLEY KAWETIRE: MBIO ZA KIPEKEE KUKUZA UTALII, AFYA NA BURUDANI MBEYA

MBEYA, TANZANIA – JUNI 28, 2025

Katika juhudi za kuhamasisha utalii wa ndani, afya njema na burudani ya kijamii, kampuni ya Mbeya 24 Tours imeandaa tukio maalum la "Fun Run – Rift Valley Kawetire" litakalofanyika tarehe 28 Juni katika mandhari ya kuvutia ya Kawetire Viewpoint, mkoani Mbeya.

Tukio hili linawakutanisha kwa mara ya kwanza wadau wa utalii, wakimbiaji wa kujifurahisha (fun runners), waendesha baiskeli na wakazi wa Mbeya na maeneo ya jirani kwa ajili ya kushiriki katika mbio za umbali wa 5km na 10km, zenye lengo la kuimarisha afya, kuleta mshikamano na kutangaza vivutio vya asili vya Tanzania Kusini.

MANDHARI YA KUVUTIA

Kawetire Viewpoint, moja ya sehemu za kipekee zinazoangalia Bonde la Ufa (Rift Valley), itatoa muktadha wa kipekee kwa washiriki, wakiweza kufurahia hewa safi ya milimani, mandhari ya kuvutia, na utulivu wa asili. Tukio hili linalenga kuwafanya watu "wakimbie kwa afya, lakini pia wagundue uzuri wa nyumbani."

KWA NINI USHIRIKI?

Mbali na mbio, Fun Run – Kawetire itajumuisha burudani mbalimbali zikiwemo muziki wa moja kwa moja, maonyesho ya bidhaa za ndani, vinywaji vya asili na chakula cha kitanzania. Washiriki wote watapata nafasi ya kujumuika, kujifunza, na kupata zawadi mbalimbali kutoka kwa waandaaji na wadhamini.

KAULI MBIU

"Kimbia, Furahia, Gundua Kawetire – Mbio siyo tu kwa ushindi bali kwa afya na urithi wa utalii."

USAJILI NA MAWASILIANO

Simu: 0714 786 087
Email: mbeya24mbeyatours@gmail.com
Instagram: @mbeya24_tours

Washiriki wanashauriwa kujiandikisha mapema kupitia mawasiliano hayo, kwani idadi ya nafasi ni ya kikomo.

Usikose! Jumuika nasi katika tukio la kipekee litakalokuacha na kumbukumbu za kudumu – Fun Run – Rift Valley Kawetire, mbio kwa ajili ya afya, utalii na burudani halisi ya Mbeya!

1 comments: