Monday, 14 July 2025

HISTORIA YA BONGO FLEVA (sehemu ya tatu): KIZAZI CHA KIBIASHARA (2010–2020)

Na Robert Eliah – burudanimbeya.blogspot.com

Baada ya miongo miwili ya misukosuko na mapambano ya kisanaa, ifikapo mwaka 2010, Bongo Fleva ilikuwa haizungumzwi tena kama harakati tu, bali kama tasnia rasmi ya burudani – iliyojitegemea, yenye mfumo, soko, na mashabiki wa ndani na nje ya nchi.

Ni kipindi hiki ambapo muziki wa Tanzania uliuza, ulivuma na kuuzwa tena – si kwa bahati, bali kwa mikakati. Hii ndiyo zama ya kizazi cha kibiashara. Na katika zama hizi, majina mawili yaliandika historia kubwa: Alikiba na Diamond Platnumz.

ALIKIBA: MFALME ALIYEKWEA KWA KIPAJI NA KIMYA CHENYE KELELE

Alikiba Saleh Kiba, aliyetambulika mapema miaka ya 2005 kupitia nyimbo kama Cinderella na Mac Muga, alirudi kwa kishindo katika miaka ya 2010, akiwa na maono mapya na utulivu wa kifalme.
Hakuwa na mbwembwe, lakini aliendesha muziki kwa heshima, ubora na utulivu akazaa hit songs kama Mwana, Aje, Chekecha, na Seduce Me akionesha Uwezo wake wa kuandika, kuimba kwa hisia, na sauti yenye utulivu wa kifalme ulimletea hadhi isiyo ya kawaida kwenye muziki wa Tanzania.

Lakini mafanikio yake hayakuishia ndani ya Tanzania. Mwaka 2010, Alikiba alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki tisa wa Afrika waliounda kundi la One8, mradi wa kimataifa wa muziki uliosimamiwa na nyota wa Marekani R. Kelly. Mradi uliowakutanisha wasanii bora kutoka Afrika. Alikiba ndiye msanii pekee kutoka Tanzania aliyechaguliwa kushiriki, akiimba pamoja na majina kama 2Face Idibia (Nigeria), Fally Ipupa (DRC) na R. Kelly mwenyewe. Huu ulikuwa uthibitisho kuwa Tanzania ilikuwa na sauti ya kimataifa, na sauti hiyo ilikuwa ni ya Kiba. Muziki wa Alikiba ulijikita kwenye misingi ya uhalisia, mapenzi ya dhati na sauti ya Afrika Mashariki. Uimbaji wake uliupa Bongo Fleva heshima.
Kupitia wimbo Hands Across the World, Alikiba akaweka jina la Tanzania kwenye ramani ya muziki wa dunia, akiwa msanii pekee kutoka nchi hii kushiriki mradi huo.
Kwa sababu hii, Alikiba anaitwa mfalme sio tu kwa sababu ya sauti yake, bali kwa heshima aliyoijenga bila kelele. Ni mfalme aliyejua kutawala kimya, lakini kila akitamka taifa linasimama kusikiliza.

DIAMOND PLATNUMZ: RAIS WA BURUDANI NA MMILIKI WA SOKO

Kama Alikiba ni mfalme wa Bongo Fleva, basi Diamond Platnumz ni rais wa burudani. Naseeb Abdul alikuja kwa kasi, akaingia sokoni kama bidhaa yenye thamani, na akapandisha thamani ya muziki wa Tanzania kimataifa.

Kutoka nyimbo kama Number One, Mdogo Mdogo, Nasema Nawe, hadi Jeje, Diamond si tu alitengeneza hits – alitengeneza mfumo. Akaanzisha Wasafi Classic Baby (WCB), lebo ya muziki iliyokuza nyota kama Harmonize, Rayvanny, Zuchu na Mbosso.
Akaanzisha Wasafi FM, Wasafi TV, na akajenga himaya ya kidijitali isiyo na mfano nchini.

Diamond ndiye msanii wa kwanza Tanzania kufikisha mamilioni ya views kwenye YouTube, kufanya collabos na wasanii wakubwa kama Ne-Yo, Rick Ross, Omarion, Fally Ipupa, na kuongoza orodha za Forbes kwa wasanii wa Afrika.

Kazi yake haikuwa tu muziki  ilikuwa ni uongozi. Akaonesha vijana kuwa burudani ni ajira, ni uwekezaji, ni utajiri. Kwa sababu hiyo, alikalia kiti cha urais wa burudani kwa kura ya mashabiki wake na kwa baraka za ushindani.

MAPINDUZI YA KIDIJITALI NA SOKO HURIA LA SANAA

Miaka hii ilishuhudia mapinduzi ya mitandao: Instagram, YouTube, Boomplay, Audiomack, TikTok. Wasanii hawakuhitaji tena redio au TV tu – sasa waliweza kujitangaza, kuuza muziki, kufanya matangazo na kuendesha biashara kupitia simu janja.

Mashindano yakazidi kuwa makali, na ubunifu ukawa silaha kuu.
Wasanii kama Vanessa Mdee, Nandy, Mbosso, Rayvanny, Harmonize, na wengine walikuja na mitindo mipya, uvaaji, video zenye ubora wa kimataifa na "branding" ya kisasa.

Sanaa ikaanza kuwa sekta ya ajira rasmi. Wasanii wakamiliki majumba, magari ya kifahari, na hata kuingia kwenye siasa, biashara na harakati za kijamii.

KIPINDI CHA MAFANIKIO, LAKINI PIA MIGONGANO

Hata hivyo, kipindi hiki pia kilijaa mikwaruzano ya kimuziki  hasa baina ya Diamond na Alikiba. Migogoro ya mashabiki, mapambano ya tuzo, na ushindani wa soko vilitawala vichwa vya habari.
Lakini katika migongano hiyo, wasanii waliendelea kukua, wakijifunza kuwa biashara ya muziki si ushindani wa nyimbo tu  ni vita ya akili, timu na maono ya mbali.

BONGO FLEVA YASIMAMA KIBIASHARA

Kipindi cha 2010–2020 ni enzi ya biashara na taasisi ya burudani. Ni kipindi ambacho muziki ulianza kupimwa kwa takwimu, mikataba, na mapato.
Wasanii wakawa CEOs, influencers, mabalozi wa kampuni na sauti za kizazi kipya.

Alikiba alionesha kuwa ubora, heshima na utulivu vinatosha kutengeneza heshima ya kifalme.
Diamond Platnumz alithibitisha kuwa ndoto, uthubutu na mikakati vinaweza kumfanya kijana wa Tandale awe mkuu wa burudani ya Afri

ka Mashariki.

Na historia bado inaendelea kuandikwa
burudanimbeya.blogspot.com
Fuata makala ijayo

0 comments:

Post a Comment