SEPTEMBA 12 – USIKU WA KIHISTORIA MBEYA
Mbeya na ukanda mzima wa Nyanda za Juu Kusini wajiandae kwa tukio kubwa la kihistoria litakalobeba uzito na heshima ya muziki unaochipua, kukua na kugusa maisha ya watu kila kona ya mikoa yetu. Tamasha la “HESHIMA YA MUZIKI WA NYANDA ZA JUU KUSINI”, linalobeba kauli mbiu ya kuinua, kuthamini na kutangaza vipaji vya ndani, linakuja kwa kishindo kikubwa kupitia jukwaa maalum ZAX THE GIANT NIGHT.
USIKU MMOJA WA KIHISTORIAUsiku wa Septemba 12, jiji la Mbeya litaandika historia mpya katika anga ya muziki. Mahali pa tukio ni Paradise Inn Hotel Outdoor – Soweto, Mbeya, ambapo wasanii, mashabiki, wadau na wakereketwa wa muziki watakusanyika kwa pamoja kuonyesha uzito wa muziki wa Nyanda za Juu Kusini.
Tamasha hili limebeba dhamira ya dhati: Kutoa heshima, kutangaza vipaji vya ndani, na kuimarisha tasnia ya muziki katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Ni usiku wa kuonesha kuwa muziki wetu una nguvu, una ladha, na una mchango mkubwa katika jamii – kiutamaduni, kiuchumi na kijamii.
ZAX THE GIANT – USIKU WA SHUJAA
Kwa mara ya kwanza, tamasha hili linamuenzi na kumtambulisha ZAX 4REAL ‘THE GIANT’ – mmoja wa sauti muhimu katika harakati za muziki wa kusini. Kupitia usiku huu, Zax atatoa burudani ya kipekee, akitumbuiza pamoja na wasanii wengine mahiri kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Iringa, Njombe, na Songwe.
Ni fursa ya kusikia muziki halisi wa nyumbani, wa mtaa, wa moyo – unaogusa maisha halisi ya watu wa kusini.
KWA NINI HUPASWI KUKOSA?
- Burudani ya moja kwa moja (Live performances) kutoka kwa wasanii wakali wa Nyanda za Juu Kusini
- Mshikamano wa wasanii na wadau – kujenga mtandao wa ubunifu na maendeleo
- Kukutana na wadau wa tasnia – wakiwemo watayarishaji, wanahabari, na ma-DJ
- Historia mpya ya muziki – fursa ya kuwa sehemu ya mapinduzi ya muziki wa kusini
MAWASILIANO
Kwa maelezo
zaidi na udhamini, wasiliana kupitia:
Simu: 0625 201 870
MWISHO WA MANENO…
Hii siyo tu tamasha, bali ni harakati. Ni sauti ya vijana wa kusini. Ni jukwaa la vipaji visivyo na nafasi. Ni heshima kwa wale waliotangulia, na mwanga kwa wale wanaokuja.
Septemba
12
Paradise Inn Hotel Outdoor – Soweto, Mbeya
Usiku mmoja wa mapinduzi ya muziki
MWAMBIE MWENZIO AMWAMBIE MWENZIE – TUKAIJAZE Paradise Inn Hotel Outdoor!
#ZaxTheGiantNight
#HeshimaYaMuzikiWaNyandaZaJuuKusini
#SasaItakuwajeeeeee
0 comments:
Post a Comment