Katika kutambua mchango wa wasanii na wadau wa sanaa kwenye ukanda wa Nyanda za Juu Kusini, Ben Royal Pictures wameibuka kidedea kwa kushinda Tuzo ya Muandaaji Bora wa Filamu kwenye Burudani Mbeya Awards 2025.
Hii ni tuzo yenye heshima kubwa
inayotolewa kwa taasisi au kampuni iliyoonesha ubunifu, uthubutu, na mafanikio
makubwa katika uzalishaji wa filamu – na kwa mwaka 2024, jina la Ben Royal Pictures limekuwa juu kwa
kila kipimo.
KIWANDA CHA UBUNIFU NA MAUDHUI HALISI
Ben
Royal Pictures wameendelea kujipambanua kwa:
-
Kuzalisha filamu zenye hadithi zenye mvuto wa
kijamii na kisasa
-
Kuwapa majukwaa waigizaji chipukizi na wakongwe
kushirikiana
-
Ubora wa picha, uhariri, na uongozaji unaokidhi
viwango vya kitaifa
-
Kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali wa Nyanda
za Juu Kusini, Ben Royal Pictures
wamefanikiwa kuunda kazi zenye athari kubwa, si tu kwa burudani, bali pia kwa
kuelimisha jamii.
SAFARI YA MAFANIKIO
Kwa mwaka 2024 pekee, kampuni hii
imeweza:
-
Kutoa filamu kadhaa zilizopata usambazaji mpana
-
Kutoa ajira kwa vijana kupitia production teams
mbalimbali
-
Kuendesha mafunzo na ushauri kwa waandaaji
chipukizi wa filamu
-
Kushiriki matamasha mbalimbali ya filamu
KUTAMBULIWA RASMI
Kwa mfumo wa upigaji kura wa Burudani Mbeya Awards (85% mashabiki, 15% academy), Ben Royal Pictures waliongoza kwa kura nyingi – ishara ya kuwa taasisi yenye mvuto, heshima, na mafanikio yanayotambulika na wengi.
Ben Royal Pictures wameonesha kuwa filamu nzuri hazitoki tu Dar es Salaam au Arusha – Mbeya nayo ina wazalishaji wa kiwango cha juu. Ushindi wao kwenye tuzo hizi ni mwanga mpya kwa tasnia ya filamu Nyanda za Juu Kusini, na ni kichocheo kwa waandaaji wengine kuendelea kuweka juhudi na ubunifu.
BURUDANI MBEYA AWARDS
2025 – KUKUTAMBUA NI HESHIMA YETU.
0 comments:
Post a Comment