Thursday 16 November 2023

AMMY CHIBA MSINGI WA T-MOTION ENTERTAINMENT

AMMY CHIBA MSINGI WA T-MOTION
Kutoka kwenye Instagram page rasmi ya T-Motion Entertainment wameandika haya

Pamoja na ukubwa aliokuwa nao Ammy Chiba na uzoefu mkubwa aliokuwa nao kwenye tasnia ya muziki lakini alikuwa ndiye msanii namba moja kwa utii na kufuata maelekezo pia hakuacha kushauri pale alipoona panahitaji ushauri kwa uzoefu aliokuwa nao. 
Alikuwa ni msanii aliyekuwa anatamani na anataka Lebo ikue kubwa Zaidi ya ukubwa alio nao yeye,hapa nanukuu moja ya ushauri ambao alishawahi kuutoa.
‘Boss unajua ninapokuwa naonekana mimi tu LEBO haitakuwa…boss naomba niwashauri vitu viwili kama vitawezekana;-
Jitahidini kuhakikisha kunakuwa na Stori matukio mengi sana yanayohusu Lebo yetu yatakayokuwa yanaongelewa kwenye vyombo vya habari,mitandaoni,mitaani na kwenye lebo zingine
Msanii hapa nisiwe peke yangu ninayehangaikiwa,nashauri wasanii wengine hapa pia wakuzwe ingawa sio kwa mara moja inaweza ikaandaliwa program nzuri isiyoumiza kwa ajili ya kuwakuza wasanii wengine pia,hii itasaidia pia mimi kutokuzubaa na itanikomaza Zaidi lakini pia kunapokuwa na ushindani kwenye Lebo ndio viwango vya wasanii vinakuwa maana kila mmoja anakuwa anataka afanye vizuri ili awe kinara wa Lebo hivyo leo inakuwa na wakali watupu na ndipo inakua. So boss tuwakuze angalau wasanii wawili
HANA UBINAFSI
Alikuwa ni msanii anayewapigania sana wasanii wenzake ambao yupo nao Lebo na hata walio nje ya Lebo,alikuwa akiona kama kuna kitu ambacho kama lebo tunaweza kufanya kwa msanii Fulani mwenye uhitaji hakusita kutushawishi kukifanya lakini akitueleza na faida tutakazopata kwa kuweza kukifanya kitu hicho. Lakini pia kwa wasanii ambao walikuwa chini ya lebo hakusita kuwaelekeza vitu ambavyo alikuwa anavijua ili wakue ikiwemo namna ya kuishi kama msanii,namna ya kuishi na viongozi wako,namna ya kuishi na wasanii wenzako,namna ya kuishi na media,namna ya kuishi na wadau wote kiujumla pia kuwafundisha kuimba alifanya sana hiyo kazi kwa wasanii waliokuwa lebo bila kujali kuwa hawa nawafundisha lakini ndio washindani wangu kwenye kazi yake.

ITAENDELEA…
https://www.instagram.com/reel/Czs_G1VNX67/?igshid=NjZiM2M3MzIxNA==

Saturday 11 November 2023

HipHop the Society

Mnamo Juni 1999, taasisi ya Uholanzi ya Madunia ilirekodi hali Halisi, Makala ya video ya dakika 30 kuhusu rap nchini Tanzania (Afrika Mashariki).

Hali Halisi "hali halisi" msemo unaonyesha rap kama chombo mbadala nchini Tanzania. Rapa na wataalamu wanatoa maoni yao kuhusu miondoko ya hip hop inayochipukia jijini Dar es Salaam na Zanzibar (Tanzania), na mawazo yao kuhusu umuhimu wa rap kama chombo cha mawasiliano.

Makala hii ilifanywa mwaka 1999 na kuachiwa mwaka 2000, hii ilikuwa ni filamu ya kwanza kurekodi matukio mahiri ya muziki wa hip hop nchini Tanzania, katika muda kabla ya BONGO FLEVA kutawala na wakati UADILIFU wa kisanii ulikuwa muhimu zaidi kuliko mvuto wa kibiashara. Inaonyesha picha za kipekee za magwiji wa vijana wa Kitanzania kama vile rapa Mr II SUGU, ambaye wakati huo alikuwa maarufu kuliko rais.

'Hali Halisi' pia ilikuwa ni asisi kwa mbinu yake ya hip hop iliyotumika kama jukwaa la elimu na majadiliano kati ya kizazi kilichotaka mabadiliko ya kweli katika siasa na jamii. Makala hiyo ya ilitunukiwa tuzo ya filamu fupi bora zaidi 'best short documentary' at New York's H2O hip hop film festival, na tuzo ilitolewa kwa watengenezaji na mc Jean Grae mbele ya magwiji wa hip hop kama vile Afrika Bambaata na Kool Herc.

Tangu wakati huo imeonyeshwa kwenye matamasha mbalimbali ya filamu barani Afrika, Marekani na Ulaya. Makala ya 'Hali Halisi' pia iliongeza msukumo mkubwa kwa mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yaligundua matumizi ya rap kama njia ya kuwasiliana na vijana.

Baadhi ya wasanii, Taasisi na watu mashuhuri walioshiriki kwenye Makala ya 'Hali Halisi':

- Kwanza Unit  

- Clouds FM

- Bonnie Luv (Mawingu studio / Clouds FM)

- Gangwe Mobb (Inspekta Haruna)

- GWM (D-Chief & KR)

- Bantu Pound (Soggy Doggy, Snaz-T)

- Mr II aka 2Proud aka Sugu

- Deplowmatz (Dola Soul aka Balozi & Saigon)

- Ras Pompidou

- Abbas & Baraka (Underground Souls)

- X Plastaz & Fortune Tellers (Arusha)

- Sos B

- P-Funk (Producer)

- Bad Gear (Coca Cola popstars)

- Mack D

- Taji Liundi (ex Clouds/Mawingu)

- Cool Para (Zanzibar)

- Sebastian Maganga (Uhuru FM)

And experts from Basata / Radio Tanzania
https://www.instagram.com/reel/CxNyzjHt4Sv/?igshid=NjZiM2M3MzIxNA==

PRODUCER MICKMER NI KURUNZI YA PRODUCTION ILIYOMULIKA KILA AINA YA MUZIKI AKIWA NA UMRI MDOGO SANA AKAWALAZA NA VIATU MANGULI ‘Atunukiwe Plaque maalum’


South side music mick mick mick mickmerr umri unakwenda miaka inasogea na kifo kinasogea… hivyo ndio wimbo wa mtafya unaitwa JE UMEJIPANGA unavyoanza kusikika nashtuka narudia tena kusikiliza jingo kwa umakini Zaidi sikio langu linaridhika kuwa nilichokisikia ndivyo kilivyo ‘South side music mick mick mick mickmerr’ nashtuka na kuingia mashaka kidogo kama huyu ninayemsikia ndio huyu Mickmerr producer ninayemfahamu mimi nikilinganisha umri alionao sasa na kama yeye ndiye aliyetengeneza huu wimbo kipindi kile na kama ni yeye je kipindi hicho umri aliokuwa nao na ukubwa wa ngoma husika ndipo nikaamua kuchukua jukumu la kutaka kupata uhakika kwa kumpigia simu.
‘Grrr grrr grrr’
Mwandishi: Micky mambo vipi?
Mickymer: Poa,inakuaje?
Mwandishi: Mungu mwema anatupigania,sorry hapa nilikuwa nasikiliza wimbo wa Mtafya unaitwa je umejipanga umetoka zamani kidogo kama sikosei ni mwaka 2012 au 2013 hivi na nimesikia kwenye wimbo huo jingo lako,vipi hii imekaaje?
Mickymer: ni mimi niliitengeneza hiyo nyimbo
Mwandishi: Hongera sana,hii habari imenishtua sana,kipindi wimbo huu unatoka miaka hiyo kama sikosei ulikuwa kidato cha pili au tatu sasa ilikuwaje kwa umri huo ukaweza kutengeneza hit song kama hiyo na ulijifunzaje funzaje kwa umri huo?
MickMer: Sikuanza kama producer na sikuwa na ndoto ya kuwa producer,ndoto yangu ilikuwa ni kuwa mwanamuziki na tulikuwa na Crew yetu iliyokuwa inaitwa REGISTAA tukiwa shule ya msingi na mimi ndio nilikuwa kiongozi. Kipindi hicho tulikuwa tunapenda sana kuimba sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye vipindi vya watoto redioni pale Mbeya fm na Generation fm,kwenye sherehe mbalimbali tulikuwa tunavamia tu bila kualikwa tunaimba pale ili mradi kujifurahisha kwasababu tulikuwa tunapenda (kwenye sherehe kama kama kipaimara na ubatizo,harusi n.k)  huu wimbo tuliimba wawili kutoka kwenye crew yetu na Fam Jizzo
Mwandishi: Endelea….
Mickmer: Tukiwa bado shule ya msingi tulifanikiwa kurekodi wimbo wetu wa kwanza kwa Producer Gwamaka Kameta (aliyetengeneza wimbo wa masanja – Kemea pepo) uliokuwa unaitwa DUNIANI na wimbo ulipigwa sana redioni na kutuongezea sana morali ya kuendelea kufanya muziki mpaka ikatupelekea kurekodi wimbo wetu wa pili kwa mtayarishaji Obbymack David alikuwa na geto studio ngoma yetu iliitwa SCHOOL.
Mwandishi: Nini kilifuata….
Mickmer: Baada ya kumaliza darasa la saba 2008 ilikuwa ni bize tu na muziki no dili no ishu yoyote hapo baadaye likanijia wazo la kuanza kujifunza kutengeneza muziki na katika kuanza kwangu kutengeneza sikufundishwa na mtu yoyote na hakuna mtu ambaye atakuja kusimama na kusema yeye kanifundisha muziki
Mwandishi: Ulianzaje sasa Uproducer?
Mickmer:Baada ya kurekodi hizo kazi kadhaa za muziki nikawa nimeona program wanayotumia (FL studio) basi na mimi nikaitafuta na kuanza kuichezeachezea na kumbuka hapo hatuna computer ila nilikuwa naenda library na jamaa zangu ingawa wenyewe hawakuzingatia sana tunalipia buku kwa lisaa then saa ikiisha naondoka mpaka siku nyingine. Muda ukaenda sana mpaka siku nilipokutana na brother Wiseman
Mwandishi: Wiseman ni nani?
Mickmer: Sitaweza kumsahau Brother Wiseman kwenye maisha yangu yote ya uandaaji wa muziki kwasababu huyu brother ndiye alinipatia fursa ya kuweza kukiendeleza kipaji changu. Ilikuwa hivi ‘Wiseman alikuwa na studio yake,kuna siku alisikia biti yangu ambayo ilikuwa trap aliipenda na kunikaribisha studio kwake na kunikabidhi niitumie kwa chochote kile bila kulipia hata senti na wakati mwingine alikuwa ananiachaia freely kabisa hata asipokuwepo,alinipao uhuru wote hapo ndipo ujuzi wangu ulikuwa mara dufu’.
Baada ya kujipika sana kwa Wiseman nikajiona sasa ninaweza kuwa producer sasa wa kuweza kuwatengenezea wasanii nyimbo rasmi basi nikaenda kwenye studio moja hivi kwa ajili ya kufanyakazi wakanipokea vizuri na pale kulikuwa na maproducer wazambia nikawa nafanya kazi pale ila wale maproducer wa pale wakawa wananitenga basi nikaamua kupiga chini na kutafuta mahali pengine.Baada ya siku kadhaa kuna jamaa akaniambia pale SouthSide wanatafuta producer so nikaamua kwenda pale na nikakutana na Danz
SOUTH SIDE MUSIC
Nilipofika South Side pale nikakutana na DANZI akanifanyia interview na wasananii watano kwa kuwarekodi na baada ya kumaliza nikajibiwa pale pale kuwa nimefaulu na kazi nimepata nikapangiwa siku ya kuanza kazi. 
Siku niliyopangiwa kuanza kazi nikafika na nikamkuta mtu mwingine aliyejitambulisha kuwa yeye ndiye Mkurugenzi mtendaji wa pale na akajitambulisha kwa jina la Aggrey.Aggrey akaniambia kuwa pale producer yupo ila basi akanifariji kwa kunipangia tarehe tofauti tofauti mpaka nikakata tamaa nikaacha kwenda. Muda ulipita sana nikawa kuna studio naitwa kama deiwaka tu mpaka siku niliyokuja kukutana kwa mara nyingine na Aggrey mtaani tu na kuanza kunishawishi niende studio. Nakumbuka siku hiyo maeneo ya Mwanjelwa tulikuwa tunahamisha vifaa kwenye saloon ya dada yangu ndipo tukakutana na Aggrey akaniambia we dogo tunakutafuta sana uje tufanye kazi ila nilimkatalia sana katakata kwasababu nilikuwa tayari nina kinyongo naye lakini alinibembeleza sana mpaka dada yangu akamsaidia kunishawishi hadi nikakubali.

KUINGIA SOUTH SIDE MUSIC
Mwaka 2011 naingia pale studio nilikuta studio imelala kabisa imepitwa na studio zote hapa mjini kwasasa (akazitaja kwa majina),mimi nataka tuirudishe hii studio kwenye ramani na naamini kwa uwezo wako wa utayarishaji tukichanganya na uwezo wangu wa kiutawala tutarudi kwenye nafasi yetu. Basi Aggrey pale pale akagawa majukumu yakwake na yakwang kama ifuatavyo:-
MAJUKUMU YANGU
Kutengeneza muziki mzuri
Mahusiano mazuri na wasanii
Kupata wasanii wakali
MAJUKUMU YAKE
Kufanya promotion
Mahusiano mazuri na media
Kufanya masoko
Kupata wasanii wakali
Kubuni contents
Rasmi tukaanza kufanyakazi na pale studio baadhi ya wasanii niliowakuta pale ni pamoja na DavyStar,Zax 4Real,Berdon n.k
KUFANYAKAZI NA MTAFYA
Kuna siku nilikuwa napita Mabatini nikamkuta Mtafya anaimba imba tu mtaani nikaona huyu mbona mkali na hastahili kufanya kimtaani taani ila kumfuata kumuambia nikawa  siwezi kumfuata ukizingatia umri wangu ulikuwa mdogo sana pia nina hali Fulani hivi ya kushindwa kumfuata mtu moja kwa moja,nikamshtua DavyStar coz niliamini yeye atamuweza na kweli Davy alimcheki na kumleta studio Mtafya na kumjumuisha kwenye familia ya SouthSide music na chap kwa haraka tukapiga mkono mmoja tu uliokwenda kwa jina JE UMEJIPANGA ambao ndio ulifungua rasmi njia ya Mtafya kwenye harakati zake za muziki.
Mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2012 tukawa tayari tumeiteka Mbeya nzima kama vile malengo yetu ambayo tulikuwa tumeyaweka na boss wangu Aggrey.
Mimi ndio producer ambaye nimefanyakazi na wasanii wote wa kizazi cha kati kile cha miaka ya 2012 mpaka 2013 kuanzia Zax 4Real,Berdon,DavyStar,Mtafya,Star boy (Piano),Samicho n.k 
Mwaka 2013 niliondoka Mbeya na kwenda dar es salaam kwa ajili ya kusoma na mishe zingine na kule nikafanikiwa kufanya kazi na maproducer na wasanii wakubwa sana ila sitaweza kuzitaja kwasababu hazina manufaa yoyote kwangu coz nilifanya kama kivuli tu.
Nje ya SOUTH SIDE MUSIC nimeshafanyakazi sehemu zingine tofauti tofauti:-
T-Motion Music – Pale wakati wanaanza anza walinichukuwa kwa ajili ya kuenda kuwapa ujuzi Zaidi na nikafanikiwa kuwatengenezea nyimbo kadhaa za Gospel na Bongo Fleva kama nne tano hivi naweza kuzitaja baadhi:-
Natamani – Meshamazing
Milele – Meshamazing
Natural woman – Ammy Chiba x Zax 4Real x Anno Melody x Fide Losso x Meshamazing
Sarafina – Zax 4Real 
Access Fm Redio – Pale nilifanya nafasi ya Redio producer
Kwa sasa natarajia kufungua studio yangu mwenyewe very soon na I promise you nyie ndio mtakuwa wa kwanza kuifahamu
KUHUSU AGGREY SOUTH SIDE
Kwa kifupi sana ‘Aggrey kwangu alikuwa ni Zaidi ya Boss Zaidi ya brother Zaidi ya mlezi Zaidi ya mshirika’

Kupitia mazungumzo haya nimegundua kuwa Mickmer: 
Ni producer aliyewatengeneza wasanii wengi sana Mbeya walionza kujulikana kwenye Generation ya 2012 na kuendelea
Hapendi na hataki kuwazungumzia wasanii ambao tayari wametoka kuwa yeye ni sehemu ya njia iliyowafikisha walipo ila kama kuna msanii atahisi kuna mchango wowote kutoka kwake yeye ndio aseme
Anaheshimu sana jitihada na kazi za producers wengine
Anapenda kule vipaji
Baadhi ya wasanii aliowahi kufanya nao kazi kwa nyakati tofauti tofauti ni Meshamazing,Annomelody,Zax 4Real,Berdon,Star Boy (Piano),Raymond (Rayvan),Danzi,DebbyCulture,Samicho,Mtafya,DavyStar na wengine

Mickmer ni versatile producer yaani chochote unachotaka anakupa iwe gospel,hiphop,bongofleva,zouk,R&B,Afro pop,singeli n.k
HipHop – Je Umejipanga – Mtafya
African zouk – Natural woman – AmmyChiba x Zax x Meshamazing x FideLosso X Anno Melody
Afro pop – Sarafina – Zax 4Real
BongoFleva – Milele – Meshamazing
N.k

Timu nzima ya Burudani Mbeya inampongeza sana na kumtakia mema kila analolifanya katika kuipeleka mbele Sanaa ya mkoa wetu.

Tuesday 31 October 2023

Usipomtaja PRODUCER DAYO ‘Dayonga’ Kwenye Orodha Yako Maproducer Wako Bora Huendi Mbinguni

Tunaweza kuwaambia nini wasanii na watangazaji wapya kuhusu producer Dayonga?
Hilo ni swali kutoka instagram page maarufu kwa habari za burudani na mitindo nyanda za juu kusini inayojulikana kwa jina la DONDOSHA NEWS.
Baada ya post hiyo watu maarufu na mashuhuri Mbeya walikuja kuweka maoni yao kama ifuatavyo;
DjDebby – ‘Mtu na nusuu…Mali safi kabisa toka kwa mzee wetu Mwambigija
VicentLaurentjrr: - ‘Dayo brotherhood toka studio ikiwa Ilolo kule katengeneza music wa wengi hawajui aisee,akiwa na Zest ,Kikunizo kabla watu hawajamjua Zax4Real kulikuwa na Zax b pembeni Ammychiba,wewe huo muziki weka mbali kabisa na watoto wa 2000 kule Nzovwe kulikuwa na Gachi b anamsuka mtu kama Trio na Rayvanny wakati huo anaitwa Raymond halafu Tunduma kuna vijana wangu Shababi International halafu kuna vichwa kama Dk Fazi na kwenye Hip hop kuna kina Makanta’
DoctorFazi: - ‘Huyu jamaa ukisikia mtu ana bifu naye basi jua huyo mtu ndio mkorofi,Dayo ni Rasta mno’
Chazdax: - ‘Hanaga noma mara ya kwanza niliweza kujuana nae studio za Mashada inc pia alikuwepo na producer Losso pale’
Bossprota: - ‘Legends Dayo plus Losso pluss Kikunizo
Comic Cliff: - Aishi milele
Baada ya kuisoma hii post na comments zake timu nzima ya burudani Mbeya ikaamua kuingia chimbo kutaka kujua huyu Dayonga ni nani hasa?
Dayonga zamani akijulikana kama producer Dayo wa Mashada inc aliyeandaliwa na Godfather wa entertainment Mbeya boss Kikunizo baada ya Zest na Losso pale mashada inc Production.
Dayo anatokea kwenye familia ya watu maarufu yam zee David Mwambigija wa jijini Mbeya yenye ndugu zake wengine maarufu kama Kikunizo Montage, Creator Pro, Criss R7 na wengine
Dayo ni miongoni mwa producer wa mwanzo kabisa wazawa walioleta mapinduzi makubwa sana ya muziki Mbeya kwa kuweza kufanya kazi nyingi zenye viwango vya hali ya juu mpaka kusababisha wasanii wa ukanda huu wa nyanda za juu kusini waache kwenda kurekodi dar es salaam na kurekodi hapahapa Mbeya.
WASANII NA WATANGAZAJI WENGI WAPYA HAWAMFAHAMU HUYU JAMAA?
Vitu vingi vilimjia kwa pamoja na kwa haraka bila kuwa na utayari
Kuanzishwa kwa mashada photo point,ikumbukwe vision nzima ya mashada inc ni ya Kikunizo hivyo baada ya kuanzishwa kwa Mashada photo point akaamua kumuachia mdogo wake Dayo studio ya muziki na wakati huo uwezo wa Dayo kwenye kusimamia studio haukuwa mzuri sana maana ilitakiwa yeye mwenyewe asimamie studio halafu afanye production then asimamie artists,promotion n.k kitu ambacho kabla alikuwa anakifanya Kikunizo. 
Kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2016 Dayo alipumzika kufanya kazi za muziki akawa anafanya shughuli zingine nje na muziki hivyo kizazi hiki cha kuanzia miaka hiyo imekuwa ngumu kidogo kumfahamu
Kwasasa Dayo ‘Dayonga’ yupo mjini Dar es Salaam akifanyakazi za muziki kwa kiwango kikubwa sana na studio kubwa na wasanii wakubwa. Zaidi tembelea insta page ya @dayonga_
Ukitaja majina matatu ya maproducer walioleta mapinduzi ya production Mbeya usisahau jina la Dayonga kwenye list yako,usipomtaja huendi mbinguni.
Credits: - DondoshaNews, VicentLaurent,DoctorFazi,Djdebby,Chazdax,Bossprota,Comic