Sunday 9 July 2017

USICHOKIJUA KUHUSU NGOMA YA KELELE YA AMMY CHIBA


KELELE ni ngoma mpya ya kwake Malkia wa nyanda za juu kusini Ammy Chiba akiwa ameshirikiana na msanii anayekuja kwa kasi sana Meshamazing a.k.a Cobra ambayo imekuwa kubwa sana redioni na kwenye mitandao ya kijamii kwa kipindi hiki.
Kuna mambo ambayo wengi hawayajui kuhusu ngoma hii na mimi nitakujuza:-
1) Ngoma hii ilitakiwa Anno Melody naye ashiriki lakini hakushiriki kwa sababu alichelewa kufika,alipofika akakuta tayari wenzie wamesharekodi verse zao na kwa maoni ya wanajopo waliokuwepo wakaona haina haja ya Anno kuingiza mistari yake maana ngoma kwa pale ilipo imekamilika tayari
2) Imeahirishwa kushutiwa mara mbili - mara ya kwanza ilikuwa ishutiwe mwezi desemba na muongozaji Tom Johns lakini ilishindikana kwa sababu ya kukosekana kwa mmoja wa wasanii (Ammy Chiba) na mara ya pili ilikuwa ishutiwe na muongozaji Cy Thor Massawe alikuja Mbeya toka Dar mwezi April lakini ilishindikana kutokana na Meshamazing kuwa shule.
3) Uandishi umefanywa na watu wanne - Ammy Chiba,Meshamazing,Necka Beatz na DoctorFazi
4) Video yake itatoka mwishoni mwa mwezi wa agosti 2017

allrightreserved@burudanimbeya

0 comments:

Post a Comment