Katika kutambua mchango mkubwa wa wadau wa burudani waliojitoa kwa moyo mmoja kuinua vipaji na kuendeleza sanaa ya mkoa wa Mbeya, Burudani Mbeya Awards 2025 imemkabidhi Tuzo ya Heshima (Lifetime Recognition Award) Dj maarufu na mdau wa burudani, Dj Aloyce George kutoka Chunya.
Tuzo hii ya kipekee imetolewa kama ishara
ya kuthamini mchango wake wa muda mrefu katika kukuza, kuendeleza, na kusimamia
vipaji vya wasanii wa mkoa wa Mbeya kwa zaidi ya miaka 15.
SAFARI YA DJ ALOYCE GEORGE
Dj Aloyce George alianza kama mdau wa
kawaida wa vyombo vya habari katikati ya miaka ya 2000. Akiwa na jina maarufu
la “Dj Anayetumia Kanda,” alianza kujulikana kupitia radio kwa kutuma salamu na
kushiriki mjadala wa mada mbalimbali redioni. Sauti yake ya kipekee, mchango
wake wa kifikra, na mapenzi yake kwa sanaa vilimfanya apate nafasi ya
kuheshimiwa na kuthaminiwa kama mdau halisi wa burudani.
MCHANGO KATIKA TASNIA YA SANAA
Katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja,
Dj Aloyce amekuwa zaidi ya shabiki – amekuwa promoter, manager, mlezi wa
vipaji, mfadhili, na muandaaji wa matamasha ya burudani. Ametumia muda, maarifa
na rasilimali zake kusaidia wasanii chipukizi na waliokomaa kwa njia
mbalimbali, zikiwemo:
-
Kuwapromoti kwenye majukwaa tofauti
-
Kuwafadhili kwenye kurekodi kazi zao
-
Kuwatafutia nafasi za kupiga shoo
-
Kuwaandalia matamasha na shughuli za kisanaa
-
Kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu maendeleo ya
kazi zao
KAULI YA KAMATI
“Tuzo hii ni kwa wale ambao wamesimama kwa ajili ya wengine. Dj Aloyce George ni alama ya kujitolea, uthubutu, na mapenzi ya kweli kwa sanaa ya Mbeya. Bila watu kama yeye, wasanii wengi wangekuwa wamepotea kabla hata ya kuonekana.”
Tuzo ya Heshima kwa Dj Aloyce George si tu zawadi binafsi, bali ni ujumbe kwa wadau wote wa burudani kuwa kujitoa kwa dhati kwa ajili ya wengine kuna nafasi na kutambuliwa. Ni heshima inayozidi maneno – ni kumbukumbu ya mchango wa kweli, unaogusa maisha.
BURUDANI
MBEYA AWARDS 2025 – KUKUTAMBUA NI HESHIMA YETU.
๐ฅ๐ฅ๐ฅ
ReplyDelete๐๐งจ
ReplyDeleteAsante
ReplyDeleteSana tena sana Nashukuru
Sana kwa hii Heshima kubwa sana kwangu.