Katika harakati za kuinua na kuendeleza sanaa ya Nyanda za Juu Kusini kupitia uandishi na uchapishaji wa habari, jukwaa la Dondosha News limeibuka kidedea kwa kushinda tuzo ya Online Media Iliyofanya Vizuri Zaidi kwa Maudhui ya Sanaa ya Nyanda za Juu Kusini katika Burudani Mbeya Awards 2025.
100% Kujitoa Kwa Ajili ya Sanaa ya Kusini
Tofauti na majukwaa mengine ya habari, Dondosha News imejikita
asilimia 100 katika kufuatilia, kuripoti na kuchambua kila tukio, harakati na
mafanikio ya wasanii wa ukanda wa Nyanda za Juu Kusini. Imechagua kuwa sauti
ya kweli ya wasanii wa mikoa ya kusini, ikitoa nafasi kwa vipaji vya ndani
kupata mwangaza na kutambulika.
Habari zinazochapishwa na Dondosha News zimekuwa:
- - Zenye mlengo wa kujenga, kuhamasisha na
kuboresha mazingira ya sanaa ya ndani
- - Zikigusa maeneo yote ya burudani ikiwemo muziki,
filamu, mitindo na sanaa nyingine
- - Zikitumia lugha ya karibu kwa mashabiki, na
kuwafanya wajisikie sehemu ya safari ya sanaa ya nyumbani
MBEYA BIG 20 – JUKWAA LINALOCHOCHEA USHINDANI NA UBORA
Moja ya mafanikio makubwa ya Dondosha News ni kuanzishwa kwa jukwaa
la MBEYA BIG 20, mp5ango unaotambua na kutangaza wasanii 20 wanaofanya
vizuri zaidi kila kipindi, na hivyo kuchochea ushindani wa ubunifu, kujituma na
ufanisi miongoni mwa wasanii wa kusini.
- Hili jukwaa limekuwa na mchango mkubwa katika:
- - Kutoa motisha kwa wasanii chipukizi na wakongwe
- - Kutengeneza rekodi ya mafanikio ya ndani kwa
uwazi na uwajibikaji
- - Kuibua mijadala na fikra mpya juu ya namna ya
kukuza sanaa ya mikoa ya kusini
DANY LOVE – AKILI KUU NYUMA YA JUKWAA
Daniel Mwakyoma, maarufu kama Dany Love, ndiye mwanzilishi na mtendaji mkuu wa Dondosha News. Uelewa wake wa tasnia, maono ya muda mrefu, na mapenzi yake kwa sanaa ya Kusini vimeifanya Dondosha News kuwa jukwaa lenye hadhi na heshima kubwa.
Ushindi wa Dondosha News ni ushindi wa dhana ya kujitegemea katika
kusimulia mafanikio yetu wenyewe. Ni uthibitisho kuwa maudhui ya kweli,
yaliyojikita kwa jamii husika, yana nafasi ya kuleta mabadiliko na kuamsha ari
mpya.
BURUDANI MBEYA AWARDS 2025 – KUKUTAMBUA NI HESHIMA YETU.
0 comments:
Post a Comment