UTANGULIZI
Mbeya Stand
Up Comedy ni jukwaa kubwa la ucheshi linalowakutanisha wapenzi wa burudani na
vipaji vya ucheshi kutoka Tanzania na nje ya nchi. Kila mwaka, tunafanya
matukio makubwa yanayovutia hadhira kubwa, huku tukiboresha tasnia ya sanaa na
burudani.
Kwa mwaka 2025, tunapanga kufanikisha Easter Comedy 2025, tukio la kipekee litakalofanyika kwa kiwango cha juu zaidi, likileta pamoja wasanii, mashabiki, na wadau wa sanaa.
MALENGO YA TUKIO
- Kutoa jukwaa la kukuza vipaji vya
ucheshi nchini.
- Kuwapatia mashabiki wa burudani
tukio la kusisimua na la kiwango cha juu.
- Kushirikiana na wadhamini katika
kukuza na kuendeleza sanaa ya ucheshi.
- Kufikia hadhira kubwa zaidi kupitia
mitandao ya kijamii na maudhui ya kidijitali.
FURSA KWA
WADHAMINI
Kama
mdhamini wa Easter Comedy 2025, unapata nafasi ya:
Kutangaza chapa yako kwa hadhira ya zaidi ya watu 1,500 watakaohudhuria
moja kwa moja.
Kufikia zaidi ya watu milioni 1+ kupitia mitandao yetu ya kijamii.
Kushiriki katika tukio lenye ushawishi mkubwa katika tasnia ya burudani
Tanzania.
Kuimarisha uhusiano na jamii kupitia sanaa na burudani.
USHIRIKIANO
NA MCHANGO WA WADHAMINI
Wadhamini
wanakaribishwa kushiriki kwa njia mbalimbali, ikiwa ni pamoja na:
- Ufadhili wa kifedha kwa maandalizi
na utekelezaji wa tukio.
- Mchango wa vifaa, huduma, au msaada
wa kimkakati.
- Ushirikiano wa kibiashara kwa
kutumia tukio kama jukwaa la kutangaza bidhaa au huduma.
HITIMISHO
Tunatoa
mwaliko rasmi kwa wadhamini wote kushiriki katika kutengeneza historia kwa
kuunga mkono Easter Comedy 2025. Pamoja, tunaweza kufanya tukio hili
kuwa moja ya matukio makubwa ya burudani nchini.
MAWASILIANO:
WhatsApp: +255 762 446 265 / +255 718 075 409
Mitandao ya kijamii: @standupcomedymbeya
#MbeyaStandUpComedy
#EasterComedy2025 #Munguametupakicheko
0 comments:
Post a Comment