MISHEK ANTONY, anayejulikana kama Necklace, ni msanii wa muziki wa kizazi kipya mwenye uwezo wa kipekee wa kufanya aina mbalimbali za muziki na kucheza (dancing). Safari yake ya muziki ilianza mitaani kama vijana wengi wanavyoanza, akijifunza na kupenda kuimba nyimbo za mitindo tofauti tofauti.
Mwaka 2020, alijiunga na kundi maarufu la Voice Brothers linaloongozwa na CEO Maswaga jijini Mbeya, hatua iliyompa fursa kubwa zaidi katika safari yake ya muziki. Baada ya kujifunza na kukomaa zaidi katika sanaa, mwaka 2023 alitoa wimbo wake wa kwanza binafsi ulioitwa "NIMERUDI", kazi ambayo ilibadilisha mtazamo wake na kumpa msukumo mpya wa kuendelea kupambana katika tasnia ya muziki.
Safari ya
sanaa haijawa rahisi kwake, kwani amekumbana na changamoto nyingi, hasa ukosefu
wa fedha na usimamizi thabiti wa kazi zake, hali iliyopelekea ugumu wa
kujiendeleza kisanaa. Hata hivyo, Necklace hakukata tamaa, na sasa
anajivunia kutangaza kazi yake mpya "IN LOVE", ambayo ni video
yake ya kwanza kabisa katika maisha yake ya muziki.
KAZI HII
MPYA – "IN LOVE"
Wimbo huu umetayarishwa na Producer Last Born kutoka BV Studio,
huku video yake ikiongozwa na Director Sir Mwifyusi. Video hii itaachiwa
rasmi tarehe 15 Machi 2025, saa nane kamili alasiri, kupitia YouTube
channel ya Burudani Mbeya.
SHUKRANI
ZA DHATI
Kwa upendo na msaada wao mkubwa, napenda kutoa shukrani za dhati kwa:
CEO Maswaga kwa kunipa nafasi ya kufanya kazi hii.
Producer Last Born kwa kutengeneza audio na kuniunganisha na director wa
video.
Director Sir Mwifyusi kwa moyo wake wa kipekee na kujitolea kuhakikisha
kuwa video hii inafanyika kwa ufanisi wa hali ya juu.
Burudani Mbeya kwa kunishika mkono na kuniwezesha kufanikisha kazi hii.
Bila sapoti
yao, kazi hii isingekamilika. Shukrani kwa mashabiki wote kwa upendo na sapoti
yenu – huu ni mwanzo wa mambo makubwa zaidi!
Hakika,
mziki ni safari, na mimi nimeamua kusonga mbele!
–
Imeandikwa na Kizz1
0 comments:
Post a Comment