RATIBA RASMI YA MATUKIO YA STANDUP COMEDY MBEYA 2025
20 Aprili
2025 – Easter Comedy Show
Tukio hili litafanyika katika kipindi cha Sikukuu ya Pasaka, likiwa na lengo la kuleta furaha na ucheshi kwa wanaMbeya wanaosherehekea sikukuu hii. Wasanii mbalimbali wa vichekesho wataonesha ubunifu wao katika kuwasahaulisha watu changamoto za maisha kupitia ucheshi.
8 Agosti
2025 – Nanenane Comedy Show
Ikiwa ni
siku maalum ya wakulima nchini Tanzania, Nanenane Comedy Show inalenga
kuleta ucheshi kuhusu maisha ya kilimo, changamoto za wakulima, na masuala
yanayohusiana na sekta ya kilimo kwa njia ya burudani. Hii itakuwa nafasi nzuri
kwa mashabiki wa vichekesho kufurahia tamasha la kipekee lenye ladha ya kilimo.
25
Desemba 2025 – Christmas Comedy Festival
Kama sehemu ya kusherehekea msimu wa Krismasi, Christmas Comedy Festival italeta burudani ya hali ya juu kwa wakazi wa Mbeya na wageni wa jiji. Hii itakuwa fursa nzuri ya kumaliza mwaka kwa tabasamu na kicheko kikubwa.
MBEYA BOY
NA TIMU YAKE YA VICHEKESHO
Jukwaa la Standup
Comedy Mbeya linasimamiwa na Stewart Asajile, anayefahamika kwa jina la
kisanii Mbeya Boy. Kupitia juhudi zake, jukwaa hili limekuwa mstari wa
mbele kuinua sanaa ya ucheshi mkoani Mbeya na kuhakikisha kuwa wasanii wa ndani
wanapata nafasi ya kuonesha vipaji vyao.
Kupitia
kauli mbiu yao, "Ukiona ratiba nyingine ujue ni wasafisha njia tu",
waandaaji wameonyesha dhamira yao ya kuwa jukwaa rasmi la vichekesho kwa mwaka
2025.
HITIMISHO
Mwaka 2025
unatarajiwa kuwa mwaka wa vicheko kwa wakazi wa Mbeya, shukrani kwa juhudi za
jukwaa la Standup Comedy Mbeya. Kwa wale wanaopenda burudani, hii ni
fursa adhimu ya kushuhudia vichekesho vya hali ya juu. WanaMbeya na mashabiki
wa vichekesho wanahimizwa kuweka ratiba zao tayari ili wasikose matukio haya ya
kipekee.
#SisindioWalewale
#MunguAmetupaKicheko
#TunamchekaShetani
0 comments:
Post a Comment