Sunday, 18 May 2025

THOBIAS MGIMWA (MR TEE KILAKA MASHINE) ASHINDA TUZO YA MWANDISHI/MTANGAZAJI BORA WA SANAA NA BURUDANI – BURUDANI MBEYA AWARDS

Katika kuwatambua wanahabari walioweka mbele sanaa na burudani ya nyumbani, jina la Thobias Mgimwa, maarufu kama Mr Tee Kilaka Mashine, limeibuka na kupewa heshima ya kipekee kwa kutangazwa mshindi wa tuzo ya Mwandishi/Mtangazaji Aliyefanya Vizuri Zaidi kwa Habari na Makala za Sanaa na Burudani katika Burudani Mbeya Awards 2025.

SAUTI INAYOINUA VIPAJI VYA KUSINI

Mr Tee ni sauti inayotambulika sana kupitia kipindi chake maarufu cha Hot Show kinachoruka kila siku kupitia Highlands FM. Kupitia kipindi hiki, amewapa wasanii wa Nyanda za Juu Kusini jukwaa la kipekee la kujieleza, kutambulisha kazi zao, na kupata maoni ya moja kwa moja kutoka kwa mashabiki. Aidha, mchango wake haujaishia redioni tu, bali pia kupitia jukwaa la mtandaoni SDP Updates, ambako amekuwa akichapisha habari, makala na matangazo yanayolenga kukuza vipaji vya ndani

SABABU ZA USHINDI

Kwa kutumia mfumo wa kura za mashabiki (85%) na kura za academy (15%), Mr Tee ameibuka kidedea kutokana na:

-          Kutoa jukwaa la kila siku kwa wasanii wa kusini, kupitia mahojiano ya moja kwa moja

-          Uchapishaji wa habari, wasifu na mafanikio ya wasanii kupitia mitandao ya habari

-          Kuibua vipaji vipya na kuviunganisha na mashabiki wao

-          Mchango mkubwa kwenye utambulisho wa sanaa ya Nyanda za Juu Kusini kitaifa

Ushindi wa Mr Tee ni ushahidi kuwa vyombo vya habari vina nafasi kubwa sana katika kukuza na kutangaza vipaji vya ndani. Yeye ni mfano wa watangazaji wachapakazi, walioamua kuwekeza muda na jukwaa lao kwa wasanii wa mikoa ya kusini.

 

BURUDANI MBEYA AWARDS 2025 – KUKUTAMBUA NI HESHIMA YETU.

1 comments: