Katika kutambua mchango wa wabunifu wa kisasa kwenye sanaa na mawasiliano ya kisanaa, Prince Graphics ametangazwa mshindi wa tuzo ya Graphics Designer Aliyefanya Vizuri Zaidi kwa mwaka 2024 katika Burudani Mbeya Awards 2025, akiwakilisha vyema ubunifu wa kidigitali kutoka Nyanda za Juu Kusini.
UBUNIFU ULIOJAA USTADI NA UMAKINI
Prince Graphics amekuwa chachu ya mabadiliko katika ulimwengu wa branding, poster design, logo creation na kazi zote za kisanaa za kidijitali. Ubunifu wake umeonekana kwenye kazi za wasanii, makampuni, matamasha na taasisi mbalimbali zilizohitaji muonekano wa kitaalamu, wa kuvutia na unaoendana na wakati.
Mbunifu huyu
ameonyesha kuwa graphics design si kazi ya nyuma ya pazia tu, bali ni sanaa
inayobeba taswira ya bidhaa au tukio lolote.
SABABU ZA USHINDI
Kwa kutumia
mfumo wa kura za mashabiki (85%) na alama kutoka kwa jopo la academy (15%),
Prince Graphics alipata alama nyingi zaidi kutokana na:
-
Ubunifu wa hali ya juu, wenye utambulisho wa
kipekee
-
Kazi nyingi zilizotumika katika matukio makubwa
ya sanaa, burudani na biashara
-
Uharaka, ubora na uaminifu katika kazi
- Mchango mkubwa katika kusaidia wasanii na makampuni kujitangaza kwa ubunifu
Prince Graphics amethibitisha kuwa wabunifu wa graphics ni mihimili muhimu wa tasnia ya burudani na biashara. Tuzo yake ni hamasa kwa wabunifu chipukizi na uthibitisho kuwa kazi nzuri huonekana, hata kama ni ya kisanaa ya nyuma ya pazia.
BURUDANI MBEYA AWARDS
2025 – KUKUTAMBUA NI HESHIMA YETU.
0 comments:
Post a Comment