Hiki ndicho alichokiandika:-
tANGAZO KWA UMMA
MIMI KALA JEREMIAH NILIKUWA MSANII WA KWANZA TANZANIA KUMSEMA
MHESHIMIWA EDWARD LOWASA KUPITIA WIMBO WANGU UITWAO WIMBO WA TAIFA
BAADA YA MHESHIMIWA KUKUMBWA NA KASHFA YA UFISADI WA RICHMOND.KWA
KIPINDI KILE KILA MMOJA WETU ALIHAMAKI SANA NA KUONA KWELI MZEE WA WATU
NI FISADI.KWENYE WIMBO HUO KUNA MISTARI NILISEMA. mi siyo mwana siasa
sisubiri tume ichunguze nistaafu ka Lowasa.
...KWA
KUWA MIMI NI MZURI SANA KWENYE KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI NILITUMIA MUDA
MWINGI SANA KULICHUNGUZA SWALA HILI LA KASHFA HII NA BAADAE NILIGUNDUA
KUWA NI SWALA LA KISIASA.NA YALIKUWA NI MAPITO AMBAYO MWANADAMU YOYOTE
HUPEWA MUDA WA KUPITIA MAGUMU ILI KUPIMWA IMANI YAKE KWA MUNGU.
BAADA YA KUGUNDUA HAYO MWAKA JANA NILITENGENEZA WIMBO UNAOITWA AZIMIO
LA ARUSHA AMBAO UPO KWENYE ALBUM YANGU YA PASAKA AMBAYO IKO SOKONI
TOKEA MWAKA JANA. KATIKA WIMBO HUO WA AZIMIO LA ARUSHA NILIANDIKA
MISTARI IFUATAYO. walipiga dili waka msakizia lowasa ili kuficha siri
kali.NILIANDIKA MSTARI HUU BAADA YA KUFANYA UCHUNGUZI NA KUJIRIDHISHA
KUWA MHESHIMIWA NI KIONGOZI BORA SANA NA HASA KWA UAMUZI WAKE WA
KUJIUZULU BILA SHINIKIZO KUBWA NA WAKATI KWA NAFASI ALIYOKUWA NAYO YA
UWAZIRI MKUU ALIKUWA NA UWEZO WA KUGOMA KUJIUZULU NA HASA KWA KUWA
HAKUWA FISADI KAMA ILIVYOSEMWA.
MWEZI WA TATU MWISHONI MWAKA
HUU NILITOA WIMBO UNAOKWENDA KWA JINA LA KARIBU DAR AMBAKO NILISEMA dar
es salam ingekuwa nchi Rais angekuwa Lowasa huku watu washashtukia kuna
mchezo kwenye siasa HAPA NILIKUWA NAMAANISHA KUWA WATU WENGI WANAOISHI
DAR WANAWAHI KUJUA MAMBO YA WANASIASA KWA KUWA WANASIASA WANAISHI HUKU
LAKINI PIA WATAFITI WENGI WA MAMBO YA KISIASA WANAISHI HUKU KWA HIYO NI
RAHISI ZAIDI KUUJUA UKWELI MAPEMA.
NAAMINI KUONDOKA KWA LOWASA KWENYE UWAZIRI MKUU KUMEZOROTESHA MAENDELEO YA TAIFA KWA KIASI FLANI
NDUGU ZANGU WATANZANIA NI WAZI KUWA LOWASA NI JEMBE TENA JEMBE LA KAZI
KUMBUKENI BILA LOWASA KUSINGEKUWA NA SHULE ZA KATA TANZANIA,NA
ANGEENDELEA KUWEPO MADARAKANI ALIKUWA NA MPANGO WA KUANZA MCHAKATO WA
ZAHANATI ZA KATA.IKUMBUKWE PIA LOWASA NDIYE ALIYESIMAMIA UJENZI WA CHUO
CHA UDOM TENA KWA PESA ZA KITANZANIA BILA KUOMBAOMBA VIMIKOPO.
MRADI WA MAJI KUTOKA MWANZA KWENDA SHINYANGA NI KAZI YA LOWASA. ZIPO
KAZI NYINGI AMBAZO NIKIZITAJA ZOTE NAWEZA KUJAZA UKURASA.NACHOJARIBU
KUSEMA HAPA NI KWA KUWA MIMI NI MSANII NA NI KIOO CHA JAMII NINGEOMBA
WEWE MWANAJAMII CHUKUA HATUA YA KUFANYA UCHUNGUZI BINAFSI KUHUSU
LOWASA.BILA KUFUATA MKUMBO WA KISIASA NAAMINI UTAKUBALIANA NA MIMI KUWA
LOWASA NI JEMBE.
MIMI HUWA NAPENDA KUSOMA VITABU VYA
WANAHARAKATI NA KUNA KITABU KIMOJA NILIKIPITIA CHA MWANAHARAKATI KUTOKA
ITALY AITWAE NICCOLO MACHIAVELLI AMBAYE ALIZALIWA MWAKA 1469 NA
KUFARIKI 1527. KATIKA ENZI ZA UHAI WAKE ALIWAHI KUANDIKA VITABU KADHAA
LAKINI KATI YA VITABU HIVYO KITABU KIITWACHO THE PRINCE NDICHO KILIMPA
HESHIMA KUBWA SANA KWA KUWA ALIIKOSOA SERIKALI YA KIFALME YA KIPINDI
HICHO KITU AMBACHO HAKIKUWA RAHISI KWA MTU KUFANYA HASA IKIKUMBUKWA
KUWA ENZI ZA UFALME ZILIKUWA ENZI ZA UBABE. KATIKA MANENO KUTOKA KWENYE
KITABU HICHO AMBAYO NINGE PENDA KUKUSHIRIKISHA WEWE NDUGU YANGU
MTANZANIA NI MANENO YAFUATAYO MACHIAVELLI ALIANDIKA HIVI. kuna kipindi
ambacho mataifa yanapita katika vipindi vigumu. na kwa kipindi hicho
kigumu mataifa hayo yatahitaji sana kupata kiongozi mwenye kuweza
kuchukua maamuzi magumu,na ambaye hatakuwa chini ya sauti ya mtu
mwingine, na ambaye ataweza kuyatekeleza maamuzi magumu kwa haraka hata
kama ni kwa kuwaumiza wachache ili wengi wawe huru.atakayekuwa tayari
kutekeleza jambo baya ili likapita na kusahaulika na atakayetekeleza
mambo mazuri kwa muda mrefu na yakaendlea kukumbukwa.kiongozi huyo
atatakiwa kuchagua kuogopwa ama kupendwa lakini ni bora akachagua
kuogopwa lakini akitenda haki kwa wananchi husika.HAYO NI BAADHI YA
MANENO ALIYOANDIKA MACHIAVELLI KWENYE THE PRINCE KITABU AMBACHO
KILIMPELEKEA KUITWA NA MFALME NA KUPEWA NAFASI YA JUU YA UONGOZI KATIKA
SERIKALI HIYO YA KIFALME.
KWA MAONI YANGU NADHANI TAIFA LETU
LIMEPITIA VIPINDI VIGUMU KADHAA NA KWA MANENO YA BWANA MACHIAVELLI
NADHANI KIONGOZI ANAYEFAA AMBAYE ANAWEZA AKACHUKUA MAAMUZI MAGUMU NA
AMBAYE HAWEZI KUWA CHINI YA SAUTI YA MTU MWINGINE NI MHESHIMIWA EDWARD
NGOYAI LOWASA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment