Wednesday, 31 July 2013

KUTANA NA ELLY L.BONKE KIJANA MDOGO MWENYE MALENGO YA AJABU-sehemu ya PILI

Elly akiwa ameshika TUZO aliyotunukiwa

Kabla hatujaendelea na sehemu ya pili tujikumbushe kwa uchache sehemu ya kwanza ilivyokuwa:,-
 Elly Lawi ni nani hasa?
Elly ni Mwanaharakati wa masuala mbalimbali ya Kiuchumi(Mjasiliamali) na Kijamii akitokea jijini Mbeya akiiwakilisha vizuri Tanzania katika ukanda huu wa Afrika mashariki.
Historia yake kwa ufupi
Amezaliwa mwanzoni mwa miaka ya tisini akiwa ni mtoto wa kwanza katika familia ye Bw & Bi Lawi yenye watoto watatu.
Elimu ya msingi ameipata katiak shule ya msingi
Halengo,Secondary amesoma Mbeya secondary School,High School amesoma Sangu Secondary School na sasa hivi ni Mwanafunzi wa chuo cha Uhasibu kilichopo Mbeya.
Harakati zake za kijamii
 Ni kiongozi na mwanzilishi wa Asasi  inayoitwa MLIMANI YOUTH GROUP inayojumuisha vijana zaidi ya hamsini(50) wa rika mbalimbali ikijumuisha vijana wanaishi nzovwe juu maarufu kama mtaa wa mlimani ndio maana ya jina la Mlimani Youth Group iliyojikita katika kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii hasa yanayogusa vijana na watoto yakilenga katika kujengeana uwezo katika kuhakikisha wanafanikiwa katika kutimiza ndoto zao kielimu,biashara,kilimo,michezo/sanaa n.k,kusaidia wasiojiweza na katika kujengeana uwezo na kuhamasishana katika kuishi kwenye misingi ya maadili mema bila kubagua dini,kabila wa jinsia.

Ni mmiliki wa organization ya EGY BUSINESS SOLUTION ambayo ni organization ya familia ikiwa ni ufupisho wa jina lake na mawili ya wadogo zake yaani Elly,Given na Yaredi.

Ni kiongozi wa kamisheni ya vijana ya shirika la YWCA Mbeya.

Ni mmoja wa wanachama wa jumuiya ya vijana ya Afrika mashariki inayoitwa CWS YOUTH ambayo inayojihusisha na masuala ya vijana  hususani kuwakomboa vijana KIFIKRA.
Malengo yake hasa ni nini?
Nilipomuuliza kuwa malengo yake ni yapi hasa alijibu 'nina lengo moja tu ambalo ni kuja kuwa Mjasiliamali mkubwa sana Tanzania na Afrika Mashariki kati na kusini'. nilipombana sana kwamba anataka kuwa kama nani akasema 'just mjasiliamali mkubwa'. Lakini akaongeza kuwa anataka siku moja jamii ije kunufaika moja kwa moja na harakati anazozifanya.

SEHEMU YA PILI-MAFANIKIO
Anasema 'kuna mafanikio yaliyopatikana kupitia harakati hizi ninazozifanya kwa kushirikiana na wanakikundi wenzangu ingawa sio kwa kiwangokikubwa sana ila namshukuru sana Mungu muweza wa yote'.Anaendelea kusema 'bila kuwa na IMANI na UTHUBUTU sidhani kama tungefika/ningefika hapa',baadhi ya mafanikio kwa uchache ni:-
1)UDHAMINI WA ELIMU-Takribani vijana kumi kutoka katika kikundi chetu wamepata ufadhili wa kusomeshwa katika ngazi ya chuo(Chuo cha Moravian Vocational Training) kwa ufadhili wa CWS YOUTH.
2)KUTAMBULIWA na KUTHAMINIWA na JAMII-kitendo cha kutambuliwa na kuthaminiwa na jamii ni mafanikio makubwa sana kwangu na huwa inanipa hamasa kubwa sana ya kuendelea katika harakati hizi ninazozifanya.
3)KUWAUNGANISHA VIJANA-Kuweza kuwaunganisha vijana zaidi ya hamsini katika mtaa wetu wa Mlimani kuwa kama ndugu na kutengeneza Mlimani Youth Group ni mafanikio makubwa sana kwangu na kikundi kwa ujumla wake.
4)Kuwapa MATUMAINI wale wote waliokuwa wamekata tamaa,kuwapa kucheka wale waliokuwa hawana furaha na kuwatia MOYO wale wote waliokuwa wamevunjika mioyo yao.
5)KUJUANA NA WATU-Kupitia hizi harakati zangu nimeweza kujuana na watu wa nyadhifa,rika,makabila na mataifa mbalimbali ambao kwa namna moja au nyingine nimeweza kujifunza mengi kupitia wao na wao pia kujifunza kupitia mimi.Mfano bila hizi harakati zangu sidhani kama hata wewe ndugu mwandishi ungekuwa unaandika kuhusu mimi muda huu.Hivyo hii kwangu ni mafanikio pia.

Pata picha za matukio mbalimba za maeneo na michezo mbalimbali kwenye bonanza waliloliandaa na kufanyika katika viwanja vya halengo

Picha ya baadhi ya member wa Mlimani Youth Group
Bango likiwa na ujumbe wa kuhamasisha kutokata tamaa
mchezo wa ready 'mdunguano'
mchezo kutembea na chupa kichwani
mchezo wa kukimbia na magunia
mchezo wa kukimbia na magunia
igizo
Viongozi wa Mlimani Youth Group








0 comments:

Post a Comment