Wednesday, 2 July 2025

JULIUS JAILO NDEJE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MBEYA VIJIJINI KUPITIA CCM.

Mbeya, 2 Julai 2025. 
Mchakato wa kuelekea uchaguzi wa ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeendelea kuchukua sura mpya leo, baada ya Julius Jailo Ndeje kuchukua rasmi fomu ya kuomba kugombea nafasi ya Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Julius Jailo Ndeje ni mmoja wa wana CCM waliobobea katika kutumikia jamii kwa moyo wa kujituma. 
Anafahamika sana kwa kuwa na mahusiano bora na wananchi, kuwa mchapa kazi, na mwenye mapenzi ya dhati na maendeleo ya jamii.
Mbali na hayo, Julius ni mlezi wa vijana na vipaji, mpenda amani, mtatuzi wa changamoto za kijamii, na zaidi ya yote ni kiongozi mwenye maono pana na anayesikiliza wananchi wake. 
Uamuzi wake wa kuchukua fomu umetafsiriwa na wengi kama hatua thabiti kuelekea kuliletea Jimbo la Mbeya Vijijini maendeleo endelevu na ya kweli.
Akipokea fomu hiyo katika ofisi za CCM Wilaya ya Mbeya, Julius alieleza kuwa lengo lake kuu ni "kuleta siasa za maendeleo, mshikamano na ushirikiano kati ya viongozi na wananchi kwa ajili ya ustawi wa kila mkaazi wa Mbeya Vijijini."
Kwa sasa, macho na masikio ya wakazi wa Mbeya Vijijini yameelekezwa kwenye mchakato huu muhimu huku wengi wakimtakia kila la heri katika safari yake ya kisiasa.

0 comments:

Post a Comment