Na Raymond George 'Ray Gee'
Leo jumamosi, tarehe 28 Juni 2025, Frank James Mwaisumbe amechukua rasmi fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini katika uchaguzi mkuu ujao.
Akiwa ni kiongozi mwenye rekodi nzuri katika kuleta mabadiliko katika jamii, Frank amekuwa mstari wa mbele katika sekta za uchumi wa vijana, burudani, ubunifu wa kijamii, na utatuzi wa migogoro, huku akijipambanua kama sauti ya kizazi kipya kinachotafuta maendeleo ya kweli yenye mshikamano na ushirikishwaji.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu, Frank amesema:
“Leo nimechukua fomu kwa imani na moyo wa utumishi. Mbeya Mjini inahitaji kasi, dira, na nguvu mpya za maendeleo—tukijenga kwa mshikamano wa vizazi vyote. Naamini wakati wa Mbeya kusimama tena kwa ari mpya ya mabadiliko ya kweli ni sasa.”
Frank amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya katika maeneo mbalimbali nchini, na pia amejulikana kwa juhudi zake kama mlezi wa majukwaa ya vijana na burudani, uchumi na maendeleo ya jamii na utatuzi wa Migogoro na ni mahiri katika kuweka msukumo katika kuwawezesha vijana kupitia uwekezaji,ujasiriamali,sanaa, ubunifu, na fursa za kisasa.
Mtazamo wake ukijikita katika kutangaza sera zinazogusa maisha ya watu moja kwa moja, zikiwemo:
- Kuimarisha uchumi wa vijana na wanawake
- Kuendeleza sekta ya sanaa na burudani kama injini ya ajira
- Kuimarisha miundombinu ya kijamii
- Kusimamia usawa na utawala bora wa rasilimali
Kwa hiliii...mm nampongeza..na hakika mbeya na tasnia ya habari(burudani) vitafikambali endapo utekelezaji utafanikiwa 🔥🔥🔥 by ray Gee
ReplyDelete