Tuesday, 15 July 2025

HESHIMA YA MUZIKI WA NYANDA ZA JUU KUSINI – ZAX THE GIANT NIGHT

SEPTEMBA 12 – USIKU WA KIHISTORIA MBEYA

Mbeya na ukanda mzima wa Nyanda za Juu Kusini wajiandae kwa tukio kubwa la kihistoria litakalobeba uzito na heshima ya muziki unaochipua, kukua na kugusa maisha ya watu kila kona ya mikoa yetu. Tamasha la “HESHIMA YA MUZIKI WA NYANDA ZA JUU KUSINI”, linalobeba kauli mbiu ya kuinua, kuthamini na kutangaza vipaji vya ndani, linakuja kwa kishindo kikubwa kupitia jukwaa maalum  ZAX THE GIANT NIGHT.

USIKU MMOJA WA KIHISTORIA

Usiku wa Septemba 12, jiji la Mbeya litaandika historia mpya katika anga ya muziki. Mahali pa tukio ni Paradise Inn Hotel Outdoor – Soweto, Mbeya, ambapo wasanii, mashabiki, wadau na wakereketwa wa muziki watakusanyika kwa pamoja kuonyesha uzito wa muziki wa Nyanda za Juu Kusini.

Tamasha hili limebeba dhamira ya dhati: Kutoa heshima, kutangaza vipaji vya ndani, na kuimarisha tasnia ya muziki katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini. Ni usiku wa kuonesha kuwa muziki wetu una nguvu, una ladha, na una mchango mkubwa katika jamii – kiutamaduni, kiuchumi na kijamii.

ZAX THE GIANT – USIKU WA SHUJAA

Kwa mara ya kwanza, tamasha hili linamuenzi na kumtambulisha ZAX  4REAL ‘THE GIANT’ – mmoja wa sauti muhimu katika harakati za muziki wa kusini. Kupitia usiku huu, Zax atatoa burudani ya kipekee, akitumbuiza pamoja na wasanii wengine mahiri kutoka mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Iringa, Njombe, na Songwe.

Ni fursa ya kusikia muziki halisi wa nyumbani, wa mtaa, wa moyo – unaogusa maisha halisi ya watu wa kusini.

KWA NINI HUPASWI KUKOSA?

-         Burudani ya moja kwa moja (Live performances) kutoka kwa wasanii wakali wa Nyanda za Juu Kusini

-         Mshikamano wa wasanii na wadau – kujenga mtandao wa ubunifu na maendeleo

-         Kukutana na wadau wa tasnia – wakiwemo watayarishaji, wanahabari, na ma-DJ

-         Historia mpya ya muziki – fursa ya kuwa sehemu ya mapinduzi ya muziki wa kusini

MAWASILIANO

Kwa maelezo zaidi na udhamini, wasiliana kupitia:
Simu: 0625 201 870

MWISHO WA MANENO…

Hii siyo tu tamasha, bali ni harakati. Ni sauti ya vijana wa kusini. Ni jukwaa la vipaji visivyo na nafasi. Ni heshima kwa wale waliotangulia, na mwanga kwa wale wanaokuja.

Septemba 12
Paradise Inn Hotel Outdoor – Soweto, Mbeya
Usiku mmoja wa mapinduzi ya muziki

MWAMBIE MWENZIO AMWAMBIE MWENZIE – TUKAIJAZE Paradise Inn Hotel Outdoor!

#ZaxTheGiantNight
#HeshimaYaMuzikiWaNyandaZaJuuKusini
#SasaItakuwajeeeeee

0 comments:

Post a Comment