Tarehe 25 Desemba 2025, Askofu wa Kanisa la Moravian Tanzania, Jimbo la Kusini Magharibi, Askofu Robert Pangani, aliongoza Ibada ya Krismasi iliyofanyika katika Ushirika wa Makongolosi, wilayani Chunya. Ibada hiyo ilifanyika kuanzia saa moja na nusu asubuhi katika hali ya ibada, utulivu na shukrani kwa Mungu, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wetu Yesu Kristo.
Friday, 26 December 2025
Saturday, 6 December 2025
BELIEVER (SIMON MLINDA) – MSALABA: WIMBO UNAOFICHUA UKWELI WA MAISHA YA MKRISTO KWA UHALISIA
Simon Mlinda, anayejulikana sasa kwa jina la kiroho Believer, ni mmoja wa wasanii wa Injili wanaojitokeza kwa nguvu na ubunifu Tanzania. Kutoka kuwa msanii wa Bongo Fleva na Hip Hop kama Green Boy, Believer ameamua kuibadilisha maisha yake, kubatizwa, na kuanza safari ya kiroho yenye uzito wa dhati.
Kwa sasa, Believer si tu msanii – ni mtumishi wa Mungu anayebeba ujumbe wa Injili kupitia muziki, ushuhuda, na ubunifu wa kisanaa.
Wednesday, 3 December 2025
HAGAI OWDEN KAMWELA (A.K.A THE PITCH): MTANGAZAJI NGULI, MBUNIFU NA MTAALAMU WA INTERVIEWS ZENYE MVUTO
Katika anga ya utangazaji na uzalishaji wa vipindi, jina Hagai Owden Kamwela, maarufu kama The Pitch, limejijengea nafasi ya kipekee. Anasifika kwa uwezo wake wa kupanga, kuongoza na kuwasilisha mahojiano yenye mvuto mkubwa, nguvu ya kushawishi hadhira, na umakini wa kipekee unaofanya mazungumzo yake kusikika tofauti. Ni miongoni mwa watangazaji wachache wanaotambulika kwa ubora wa hali ya juu katika kufanya interviews zenye kina, hadhi na ubunifu.
Safari ya The Pitch imekuwa msururu wa juhudi, bidii na mafanikio yaliyopimwa kwa matokeo anayoacha kila mahali anapopita.
MWANZO: BIG STAR FM – MBEYATuesday, 18 November 2025
JACKSON ANANGISYE: UVUMILIVU, BIDII NA MAFANIKIO YALIYOONEKANA
Jackson Anangisye Mtafya ni kipaji kinachoendelea kuangaza katika tasnia ya utangazaji nchini Tanzania. Alizaliwa na kukulia Songwe, eneo lililojulikana zamani kama Ileje, na safari yake ya utangazaji imejengeka kwa uvumilivu mkubwa, bidii, na dhamira thabiti ya kufanikisha ndoto zake.
Wednesday, 5 November 2025
MESHAMAZING AACHIA WIMBO MPYA “REVERSE”, AONYESHA UBORA NA UTAMBULISHO HALISI WA MUZIKI WAKE
Na Burudani Mbeya Media
Msanii nyota Meshack Fukuta maarufu kama MeshAmazing, ameendelea kuthibitisha kuwa ni miongoni mwa vipaji vinavyochangamka zaidi kwenye muziki wa Bongo Fleva baada ya kuachia rasmi wimbo wake mpya unaoitwa “Reverse”.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, MeshAmazing alitangaza ujio wa ngoma hiyo kwa maneno ya shukrani akisema:
“Mungu mwema tupo salama Ngoma yetu Tayari ipo YouTube, link ipo bio.”







.webp)
