Tuesday, 29 July 2025

NAY WA MITEGO AVAMIA TUNDUMA KWA KISHINDO: “TUNDUMA NI MOJA YA NGOME ZANGU KUBWA KABISA!”

Tunduma, Tanzania – Katika mwendelezo wa #BachelaTourSeason2, msanii nguli wa muziki wa Bongo Fleva Emanuel Elibariki, maarufu kama Nay wa Mitego a.k.a NayTrueBoy, amefanya onyesho la kihistoria lililotikisa mji wa Tunduma usiku wa Jumamosi, na kuacha alama isiyofutika katika mioyo ya mashabiki wake.

Akihutubia maelfu ya mashabiki waliokusanyika kwa shangwe na nderemo, Nay alieleza wazi mapenzi yake kwa Tunduma kwa kusema:

“Tunduma ni moja kati ya ngome zangu kubwa kabisa! Mimi ndiye Rais ninaependwa zaidi duniani na wananchi wangu kuliko Rais yoyote yule. Hili halina ubishi!”

Kauli hiyo imeamsha hisia kali mitandaoni huku mashabiki wengi wakimpongeza kwa kuendelea kuwakilisha ukweli wa mtaa na sauti ya walio kimya. Onyesho hilo lilijaa burudani, ujumbe, na mawasiliano ya moja kwa moja kati ya Nay na mashabiki wake, jambo ambalo limekuwa kiini cha mafanikio ya Bachela Tour.

Mbali na kutumbuiza kwa moto wa nyimbo zake maarufu kama “Rais wa Kitaa,” “BACHELA,” na “Makuzi,” Nay alitumia fursa hiyo pia kuwashukuru mashabiki wake wa Tunduma kwa mapokezi ya kishujaa.
“Tunduma asanteni sana! See you next time my people. Mmenipa nguvu mpya ya kuendelea na hii mission ya kweli.”

KUHUSU #BACHELATOURSEASON2

Bachela Tour ni mfululizo wa matamasha yanayoandaliwa na Nay wa Mitego yenye lengo la kuwafikia mashabiki wake moja kwa moja mtaani, “chaka kwa chaka,” akileta burudani, hamasa, na ujumbe wa kweli bila madoido.

Kwa mashabiki wa Nay, #BachelaTourSeason2 si tu burudani ni harakati. Ni mwamko wa kisanaa unaoongozwa na msanii asiyeogopa kusema ukweli, bila hofu wala kuyumba.

Tunduma mmekuwa historia. Mnakumbukwa!
Nay wa Mitego – NayTrueBoy. Bado tupo mtaani.

#BachelaTourSeason2
#ChakaToChaka
#RaisWaKitaa
#Tunduma

0 comments:

Post a Comment