Muziki wa Hip Hop na Bongo Fleva nchini Tanzania umejikita si tu katika burudani, bali pia katika utoaji wa ujumbe, hisia, na msimamo. Moja ya njia ambazo wasanii wamekuwa wakitumia kueleza hisia zao au kutatua tofauti zao ni kupitia "Diss Tracks" — nyimbo ambazo hulenga kumkejeli, kumkosoa, au kumshambulia msanii au mtu maarufu mwingine, aidha kwa njia ya moja kwa moja au kwa kutumia maneno ya mafumbo (subliminals).
Kuanzia miaka ya mwishoni mwa 1990 hadi sasa, Tanzania imekuwa na matukio kadhaa ya beef kati ya wasanii, na baadhi ya matukio haya yamezaa nyimbo kali za dissing zilizotikisa anga ya muziki. Makala hii inaangazia baadhi ya diss tracks maarufu za Kibongo, ikifichua chimbuko la mivutano hiyo, mistari ya kufokewa, na athari zake kwa game la Bongo Fleva.1. "MTULIZE" – MABAGA FRESH (DISSING GANGWE MOBB & INSPECTOR HAROUN)
Kama kuna diss track ya mwanzo kabisa iliyoweka msingi wa vita ya maneno kwenye Bongo Flava, basi ni "Mtulize" ya Mabaga Fresh. Katika wimbo huo wa mwaka 2000, Mabaga Fresh walimshambulia waziwazi Inspector Haroun na kundi lake la Gangwe Mobb kwa mistari ya kejeli iliyotokana na ugomvi wa malipo duni kwenye show ya Temeke.
Chanzo cha Beef:Beef kati ya Mabaga Fresh na Gangwe Mobb kilianzia kwenye show ya Temeke mnamo 1999 ambapo Gangwe Mobb walitapeliwa malipo yao na kuambulia shilingi 500 tu baada ya show yenye mafanikio. Mabaga Fresh walidai kuwa walipata hasara, jambo lililowakasirisha Gangwe.
Mistari ya DISS:
- JB: “Mbele ya chombo cha dola hakuna cha Ngangari” – Akiponda jina la wimbo maarufu wa Gangwe Mobb.
- DJ Snoxx: “Ngedere niazime sura yako nimtishie mwanangu” – Dongo kali kwa Inspector Haroun akidokeza sura yake.
2. "NIPO GADO (ORIGINAL)" – INSPECTOR HAROUN FT. ZAY B (DISSING JB WA MABAGA FRESH)
Chanzo
cha Beef:
Wimbo huu ni jibu kwa disstrack ya "Mtulize". Haroun aliamua kumtumia
Zay B kutoa majibu kwa mistari ya JB.
Mistari ya DISS:
- Zay B: “Kubwa zima kikojozi, ukiulizwa ooh nimepitiwa na njozi” – Dongo la moja kwa moja kwa JB, akiparodi mstari wa "Mtulize".
- Inspector: “Mi ndo nyani wa mwituni porini, stering” – Kujibu dongo la kumfanana na ngedere, akijinasibu kama kiongozi wa porini.
3. "NIPO GADO REMIX" – ZAY B & JUMA NATURE (DISSING INSPECTOR HAROUN)
Chanzo
cha Beef:
Zay B na Juma Nature waliamua kumchana Inspekta hadharani kutokana na tofauti
zao za kisanaa na mitazamo.
Mistari ya DISS:
- Zay B:
ü “Domo ka chai jaba” – Anamkejeli kwa muonekano wake.
ü “Watu hawachoki wamenuna, wamechoshwa na urembo wa sanaa” – Akikosoa staili ya kurap ya Inspekta.
ü “Mi nahisi wenzako wanakugonga” – Matusi ya moja kwa moja.
- Juma Nature: Hali ilizidi kuwa tete pale Juma Nature aliposhiriki katika remix hiyo huku akiingia kwenye mgogoro wake binafsi na Inspector kuhusiana na nani aliyekuwa wa kwanza kutumia style ya kuchana kwa lafudhi ya mitaani.
ü “Sumbua akili kijana, usiniige mimi utalost” – Akisisitiza kuwa Inspekta anamwiga, na si msanii halisi.
4. COMPLEX (R.I.P) – DISS KWA GANGWE MOBB
Chanzo
cha Beef:
Complex alikuwa mshirika wa karibu wa Zay B, hali iliyomuweka kwenye mgogoro na
Gangwe Mobb.
Mstari wa DISS:
- “Nimekwisha pita vyeo vyote, uinspekta na uluteni, now I'm a field marshall so you better salute me” – Akipunguza hadhi ya majina ya Gangwe (Inspector & Luteni).
5. "VIDONGE VYAO" – GANGWE MOBB FT. NASMA KIDOGO (DISSING ZAY B & JUMA NATURE)
Chanzo
cha Beef:
Gangwe walihisi wasanii kama Zay B na Nature waliwapiga vita kwa fitna na
kujaribu kupanda kwa kutumia jina la Inspekta.
Mistari ya DISS:
- “Kupanda chati kwa jina la Inspekta Haroun watu wanaanza kuponda” – Wakieleza kuwa mafanikio ya wasanii waliokuwa karibu na Inspekta ni matokeo ya kutumia jina lake.
6. "JINSI KIJANA" – JUMA NATURE (DISSING INSPECTOR HAROUN)
Chanzo
cha Beef:
Huu ulikuwa mfululizo wa beef yao iliyokuwa wazi, hasa baada ya malumbano yao
kwenye vyombo vya habari. Nature alimtuhumu Inspekta kuwa mbinafsi na
asiyependa kushirikiana na wengine.
Mistari ya DISS:
- “Vurugu zako za siri kuwa ni mtu ubinafsi” – Akimkosoa kuhusu tabia ya kutotaka kushirikisha wengine.
- “Adui mfano wa nduli kakosa tabia nzuri” – Akitilia mkazo kwamba Inspekta ni mtu mgumu kuelewana naye.
- “Najua inakuuma moyo unaposikiliza hili song, unatamani uzime redio, usisikilize mi sichongi” – Dongo la mwisho la kushusha presha na kumdharau Inspekta.
Diss tracks zimekuwa sehemu muhimu ya historia ya muziki wa Bongo Fleva, zikichangia si tu burudani bali pia mazungumzo na ushindani wa kisanii. Huku baadhi ya beef zikimalizika kwa maridhiano, zingine zilibaki kuwa kumbukumbu ya mapambano ya kisanaa yaliyobeba vionjo vya ubunifu, ukali wa maneno, na mapambano ya umwamba. Hakika, disstracks hizi si tu zilitikisa anga ya muziki, bali pia ziliwajenga au kuwavuruga baadhi ya wasanii katika tasnia.
ITAENDELEA…
0 comments:
Post a Comment