Tuesday, 16 July 2013

TABIA TISA (9) ZA WATANZANIA ZINAZOKERA ZAIDI

1. Kwenda haja ndogo na kubwa hovyo...
Hivi huwezi kuwa mstaarabu na kutafuta msala wa karibu walau hata kwenye bars au hata gas stations?
Yaani kuna sehemu ni maarufu kwa watu kumwaga oil zao tena bila hata aibu...Hebu tuwe wastaarabu bhanaaa...

2. Watu wanayopayuka ndani ya daladala, ndege na vyombo vingine vya usafiri...
Utakuta mtu anaongea kwa sauti kubwa kama Sued Mwinyi anatangaza mechi baina ya Yanga na TP Lindanda wana Kawekamo ya kina George Masatu...
Mmoja yupo nyuma na mwingine yupo mbele kabisa, wanasogoa weee wakati huenda mbali na kutumia lugha zao za asili...omba Mungu kisiwe Kisandawe au Kimasai(huu ni mfano tu)...

3. Wanaume ambao hata wakikuona upo na dada yako wanadhani ni kimada...
Hawa huwa wananikera hakuna mfano, "shemeji kap
endeza" mara nyingi hiyo ni moja ya kauli za watu kama hawa...
Pia wapo wale wengine ambao huenda mbali zaidi na kuazna kupiga miluzi au kutoa machombezo yenye kuashiria matamanio ya kingono...

4. Wale wote wanaotupa hovyo uchafu...
Mtu umemaliza kunywa maji yako ya uhai, au Kiroba n.k...kwa nini usihifadhi hicho kifungashio na ukakiwage sehemu stahiki mbele ya safari...
Yaani sisi Watanzania sijui lini tutajifunza kutumia akili....ndio maana kuna vitu vingi nadhani Mungu kaamua kutunyima kwa sababu ya tabia zetu za ajabu ajabu...

5. Makonda waonyanyasa wanafunzi...
Hawa watu sijui hawajawahi kwenda shule au ni ulimbukeni! Yaani wasimuone mwanafunzi anasogelea gari, kirahisi tu utasikia "Oyaa limeshajaa"...
Magari yenyewe hata sio yao na wala hawana ndoto za kuwa na magari miaka 900, lakini ni watata zaidi ya utata wenyewe.

6.Kuchokonoa pua
kuchokonoa chokonoa pua mbele ya watu..af akimaliza anakupa mkono huo huo msalimiane au muagane.
7.Kutokujali muda
katika tabia zinzokera hii mimi nafikiri inanikera zaidi. mtu umeacha kazi zako ili utimize promise ya muda mliopangiana, halafu yeye unakuta analeta za kuleta, anakukalisha lisaa lizima ukimsubiri, halafu akifika analeta masikhara ya oooh si unajua time zetu za kiswahili...yan huwa natamani kumtwanga vichwa vya utosi...
kama huwez ku-keep time sema mapema kuliko kupotezea wengine muda na kuwaharibia ratiba zao.
8.Kuvaa nguo zisizo na staha kanisani
Baadhi ya akina dada kwenda makanisani na nguo zisizi na staha.... yaan utakuta kavaa kinguo kifupi hadi aibu, mwingine mabega wazi au nguo ndefu ila imebana afu ya kitambaa cha poliesta.... Kha!!!!!
9.Chabo za chatting
Mmekaa kwenye foleni say unachat na wana kupitisha time kuna boya katoa mimacho kwenye simu yako anasoma kila kitu,yaaani mpaka ukikosea kuandika NYUMBA anatamani akuambie sio numba ni nyumba khaaaaaaaaaaaa!!!!!!
Dawa ni kuandika; NINAYE HAPA KAKAA UPANDE WANGU WA KULIA/ KUSHOTO NA NTAMFUATILIA NIJUE ANAPOKAA ILI USIKU TUMALIZE ILE ISHU

0 comments:

Post a Comment