Mh.SUGU
Mbeya. Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, (Sugu)
(Chadema) ameendelea kumkalia kooni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuhusiana
na kauli aliyoitoa bungeni ya kuruhusu polisi kuwapiga raia ambapo
alidai kwamba hakupima kauli na wadhifa wake wakati akitoa kauli hiyo.
Sugu alitoa kauli hiyo juzi kwenye mkutano wa
hadhara wa Chadema uliofanyika Mji Mdogo wa Mbalizi nje kidogo na Jiji
la Mbeya wakati akiwahutubia wakazi na wafuasi wa chama hicho.
Alisema kamwe hawezi kufuta kauli na
maneno yake aliyoyatoa kwenye mtandao wa kijamii akimtuhumu Pinda kwa kauli yake na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa kama huyo.
maneno yake aliyoyatoa kwenye mtandao wa kijamii akimtuhumu Pinda kwa kauli yake na haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa kama huyo.
“Kauli aliyoitoa Pinda bungeni kamwe haikubaliki
na mwananchi yoyote na ndiyo maana hata mimi nilisema na nitaendelea
kumsema Pinda kwa kauli zake hadi pale atakapowaomba radhi Watanzania,”
alisema Sugu na kuongeza:
Alisema ili kujisafisha kuhusiana na kauli yake
yenye lengo la kuwanyanyasa Watanzania ni lazima awaombe radhi na kama
hatafanya hivyo basi ajiuzulu wadhifa wake.
Alisisitiza kwamba kamwe hatasita kusema jambo kwa
masilahi ya wanaMbeya na Watanzania kwa jumla,kwa kuogopa vitisho vya
vyombo vya dola kama walivyotaka kumchukulia hatua baada ya kumsema
Pinda kupitia mitandao ya kijamii.
Source:gazeti la Mwananchi
Source:gazeti la Mwananchi
0 comments:
Post a Comment