SEPTEMBA 12 – USIKU WA KIHISTORIA MBEYA
Mbeya na ukanda mzima wa Nyanda za Juu Kusini wajiandae kwa tukio kubwa la kihistoria litakalobeba uzito na heshima ya muziki unaochipua, kukua na kugusa maisha ya watu kila kona ya mikoa yetu. Tamasha la “HESHIMA YA MUZIKI WA NYANDA ZA JUU KUSINI”, linalobeba kauli mbiu ya kuinua, kuthamini na kutangaza vipaji vya ndani, linakuja kwa kishindo kikubwa kupitia jukwaa maalum ZAX THE GIANT NIGHT.
USIKU MMOJA WA KIHISTORIA